MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kagae: Waziri Mkuu Ajaye Atamsaidia Rais Samia Kuongeza Kasi ya Maendeleo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kagae: Waziri Mkuu Ajaye Atamsaidia Rais Samia Kuongeza Kasi ya Maendeleo
Habari

Kagae: Waziri Mkuu Ajaye Atamsaidia Rais Samia Kuongeza Kasi ya Maendeleo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Exaud Kagae, amesema ana matumaini makubwa kuwa, Waziri Mkuu ajaye atakuwa kiongozi thabiti, mwenye dira na uwezo wa kusimamia ajenda kuu za maendeleo ya taifa.
Kagae amesema hayo leo Novemba 12, 2025 katika viwanja vya Bunge alipozungumza na Waandishi wa Habari, ambapo kesho Novemba 13, 2025 bunge linaenda kuthibitisha jina la Waziri Mkuu ajaye.
Habari Picha 10269
Amesema uteuzi wa Waziri Mkuu ajaye ni hatua muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo ya Taifa ya 2020 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambayo ndiyo msingi wa serikali inayoundwa.
“Tunatarajia kupata Waziri Mkuu atakayesimamia ajenda za kitaifa kwa ufanisi, atakayehakikisha maendeleo endelevu yanafikiwa na kumsaidia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza kasi kubwa ya maendeleo tuliyoiona katika miaka minne iliyopita,” amesema Kagae.
Akimpongeza Rais Samia kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi chake cha uongozi, Kagae amesema maendeleo hayo yameleta mabadiliko makubwa hata katika jimbo lake la Mufindi Kaskazini.
“Ninakiri wazi kwamba mafanikio ya serikali ya awamu ya sita yamenisaidia sana katika jimbo langu. Tumetekeleza miradi mikubwa ya kihistoria, kuanzia ujenzi wa barabara za lami vijijini, upatikanaji wa maji safi, kuboreshwa kwa huduma za afya na elimu, hadi miradi ya miundombinu inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja,” amesema.
Mbunge huyo amesema ana imani kuwa Waziri Mkuu ajaye ataendeleza kasi hiyo ya maendeleo, kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati, na kuleta tija kubwa zaidi kwa wananchi.
“Tunataka kiongozi ambaye atakuwa bega kwa bega na Rais Samia kuhakikisha maendeleo yaliyopatikana katika miaka minne iliyopita yanaongezeka mara mbili zaidi. Hii itawezekana tu kwa Waziri Mkuu jasiri na mwenye ufuatiliaji makini wa kazi za serikali,” amesema.
Kagae pia aliwashukuru wananchi wa Mufindi Kaskazini kwa ushirikiano waliomuonyesha katika kipindi kilichopita na kuahidi kuendelea kushirikiana nao kwa ukaribu katika muhula huu wa pili.
“Ninawashukuru wananchi wangu kwa kuniunga mkono kwa dhati. Tumeanzisha miradi mikubwa ambayo haijawahi kufanyika, na naamini katika kipindi cha 2025 hadi 2030 tutazidi kufanikisha zaidi. Wakati huu tutazidi kuandika historia ya maendeleo katika jimbo letu,” amesema.

You Might Also Like

UDSM Yabuni Teknolojia Mpya ya Kuhesabu Samaki Kwa Haraka 

WCF Yaleta Utulivu Mahala Pa Kazi – Katambi

Serikali  Kuja Na Mradi  Wa Kuimarisha Upatikanaji Umeme Vitongojini- Kapinga 

Simbachawene Asema Serikali Yajivunia Mafanikio TASAF

Kisaro Ahojiwa Kuhusu Migogoro ya Ardhi,  Mwinje Ajitosa na Suluhisho la Miundombinu na Umiliki wa Ardhi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mbunge Ndoinyo Kubadilisha Taswira ya Ngorongoro Na Kuimarisha Utalii, Ufugaji
Next Article Munde Aahidi Kuboresha Miundombinu, Uchumi Wa Liwale
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?