Na Lucy Ngowi
MOROGORO: WAANDISHI wa Habari nchini Tanzania wametakiwa kuandika na kutangaza habari za vyama vyote kwa usawa,.
Aidha Vyama vya Siasa vimetakiwa kutoingilia uhuru wa vyombo vya habari.
Mwenyekiti wa JChama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari Tanzania ( JOWUTA),,Mussa Juma ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya waandishi wa habari Kanda ya Mashariki na Pwani yaliyofanyika mkoani Morogoro leo April 24,2025.
Juma amesema, kuelekea uchaguzi mkuu,.wanahabari nchini wanapaswa kutenda haki kwa vyama vyote vya siasa.
“Tunataka katika Uchaguzi Mkuu ujao wanahabari tuzingatie sana maadili,tuache ushabiki wa vyama na wale wenye mapenzi na vyama bora wajiweke kando katika tasnia hadi uchaguzi upite,” amesema.
Akitoa mada juu ya ulinzi na usalama kwa waandishi wakati wa uchaguzi,Juma amewataka wanahabari kujali usalama wao na usalama wa vyombo vyao vya kazi wakati wa uchaguzi na kabla.
“Kabla hujaandika habari fanya tathimini ya habari yako,inawagusa kina nani,je ina athari gani na kama inavitisho chukuwa tahadhar,” amesema
Naye Ofisa Uchaguzi wa Manispaa ya Morogoro,Shabani Duru akifungua mafunzo hayo amewataka waandishi wa habari kufanyakazi kwa weledi kuelimisha umma masuala ya uchaguzi.
Duru anesema, wanahabari ni wadau muhimu katika.uchaguzi mkuu na wataendelea kushirikisha katika mchakato wote wa uchaguzi.
Mwakilishi wa Mtandao wa watetezi wa haki za Binadamu (THRDC), Wakili
Jons Sendodo akitoa mada juu ya sheria za uchaguzi na kuripoti habari.za uchaguzi amewataka wanahabari kuzijua sheria lakini kuzingatia ukweli,Usahihi na masuala ya jinsia.
Wakili Sendodo, amewataka wanahabari kutambua umuhimu wa usalama.wao kazini na kujua kuna vyombo vya kuwatetea wanapokabiliwa na majanga.
Naibu Katibu Mkuu wa JOWUTA, Said Mmanga akitoa mada juu ya maadili ya uandishi kuelekea uchaguzi mkuu, amesema maadili ya waandishi muhimu kuzingatiwa.
Amesema kuelekea uchaguzi ni vizuri waandishi kuandika ukweli,kujiepusha na habari za uzushi na upendeleo na upotoshaji.
Mafunzo hayo ya wanahabari yanaendelea katika mikoa ya Mbeya,Iringa na Njombe na baadae Arusha kwa waandishi wa Kanda ya Kaskazini.