MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: JMAT Yatoa Neno Yanayoendelea Kwa Vijana Wa Kenya
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > JMAT Yatoa Neno Yanayoendelea Kwa Vijana Wa Kenya
Habari

JMAT Yatoa Neno Yanayoendelea Kwa Vijana Wa Kenya

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Danson Kaijage.

DODOMA: JUMUIYA ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), imeeleza kusikitishwa na yale yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii hasa kwa vijana wa Kenya kumvunjia heshima Rais Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Shekhe Dkt. Alhad Mussa Salum, amesema hayo jijini hapa, alipokuwa akitoa tamko la taasisi hiyo kwa waandishi wa habari.

Amewaomba viongozi wa dini na wale wa kiasisa nchini Kenya kuzungumza na vijana hao kuacha kumvunjia heshima Rais Samia.

“Sisi tunaamini Kenya ina viongozi wa dini lakini kuna viongozi wa serikali tunawaomba sana tuwasihi vijana wetu hawa waone angalau heshima ya kiongozi wa Taifa jingine ikiwemo Tanzania.

“Tuwakumbushe heshima ya taifa lolote ni maadili ya watu wake kama Wakenya wataendelea na matusi ni dhahiri itakuwa ni kumkosea sana Mwenyezi Mungu kuwatukanisha wazazi wao pia na kupoteza ustarabu katika uso wa dunia kwa Taifa hilo,”amesema.

Amesema Wakenya na Watanzania bado wanahitajiana hivyo sio jambo jema linalofanywa na vijana hao.

“Tulipofika panatosha kwani moto mkubwa huanza kama cheche ndogo hivyo ipo haja ya kuzizima cheche hizi kabla haujawa moto mkubwa,”amesema.

Katika hatua nyingine amempongeza Rais Samia kwa kuonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa katika kadhia hiyo.

“Mama au mwanamke huzaa watoto tofauti tofauti siyo wote wanaweza kupata maadili mema lakini wote ni watoto, vijana wa Kenya ni watoto waliozaliwa na mwanamke vijana wa watanzania ni watoto waliozaliwa na mwanamke mama samehe mtoto wa mwenzio ni wako.

“Tunamkumbusha mama Samia yaliyompitia masiha Yesu mwana wa Mariam ni makubwa zaidi, lakini alisamehe saba mara sabini, aliyofanyiwa Mtume Muhammad mabaya makubwa lakini aliwaambia waliomfanyia vibaya nendeni nanyi mko huru,”amesema.

Ameipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kutumia hekima na busara nyingi katika kuyaendea mambo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Wizara na vyombo vyetu mbalimbali vya usalama vina heshima kubwa katika kumlinda mtanzania na mali zake, heshima ya viongozi wake na amani ya Tanzania kwa ujumla,”amesema.

Amesema Kenya inahitaji Amani, Tanzania inahitaji Amani hivyo wanaomba viongozi wenzao wa dini nchini humo kushirikiana katika kuwaongoza na kuwashauri vijana wao kuheshimu na kutovunja mahusiano mazuri waliyoyajenga kwa miaka mingi.

 

 

 

You Might Also Like

Watu Zaidi Ya 3500 Wapatiwa Huduma Ya Kisheria Wizara Ya Katiba Na Sheria

Zitumieni fursa za misitu na nyuki-Tafori

Mama Janeth Magufuli Atembelea Banda La Ofisi Ya Waziri Mkuu Sabasaba

  Tanesco Yagawa Zawadi Ya Majiko Sabasaba Kuhimiza Matumizi Nishati Safi

Maadhimisho Ya VETA Ya Miaka 30 Kuhitimishwa Machi 18 Hadi 21, DSM

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Miaka Minne Ya Samia Na Sekta Ya Elimu
Next Article Kafulila: Deni La Taifa Ni Himilivu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mara Yapaa: Miaka Minne Ya Mafanikio Chini Ya Rais Samia
Habari July 18, 2025
Serikali Yazindua Mafunzo Ya Mtandao Ya Afya Moja
Habari July 16, 2025
Ubunifu Na Kufanya Tafiti Kwawezesha UDOM Kupokea Tuzo
Habari July 16, 2025
Utafiti Wa Nguvu Kazi, Mapato Ya Kaya Kutoa Taswira Mpya Ya Maendeleo
Habari July 15, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?