MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Imarisheni Mkakati Wa Kusimamia Usafi Wa Mazingira-Mhagama
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Imarisheni Mkakati Wa Kusimamia Usafi Wa Mazingira-Mhagama
Habari

Imarisheni Mkakati Wa Kusimamia Usafi Wa Mazingira-Mhagama

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama amesema ili kuepuka magonjwa ya mlipuko ameagiza Idara ya Kinga Wizara ya Afya kuimarisha mpango mkakati wa kusimamia suala la usafi wa mazingira katika majiji makubwa pamoja na maeneo ya mipakani mwa nchi.

Waziri Mhagama amesema hayo leo Septemba 9, 2024 wakati wa kikao na Idara ya Kinga Wizara ya Afya kwa lengo la kujadiliana utendaji kazi wa idara hiyo pamoja na kujua majukumu ya Idara hiyo.

“Tukumbushane kuzingatia usafi, kuanzia katika mikoa mikubwa (majiji) kama vile mkoa wa Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Mwanza pamoja na mipakani hii itaweza kusaidia mikoa mingine kuiga mfano huu na hatamaye tutafanikiwa nchi nzima.” Amesema Waziri Mhagama

 

Aidha, Waziri Mhagama ameelekeza kutengenezwa kwa programu maalum ya kusimamia suala la matumzi ya vyoo bora ambavyo vitatumika kwa ufasaha ili kudhibiti magonjwa ya mlipuko na kuleta usalama wa afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Ntuli Kapologwe wakati akiwasilisha taarifa yake amesema, afya ya mazingira inajumuisha afua zinazolenga kuzuia visababishi vya magonjwa ambapo afua hizo ni pamoja na usafi wa mazingira, udhibiti wa wadudu wadhurifu na wanyama waharibifu.

“Lakini pia afua nyingine ni pamoja na udhibiti wa taka, usalama wa chakula, usalama wa maji ya kunywa, udhibiti wa magonjwa mipakani, huduma za Afya mahala pa kazi pamoja na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira.” Amesema Dkt. Ntuli

Idara ya Kinga inajukumu la kuandaa sera, sheria, kanuni na miongozo ya huduma za afya kinga na kusimamia utekelezaji wake, kuandaa na kusimamia utoaji wa elimu na hamasa katika masuala ya Afya kwa umma, kuratibu na kukuza utafiti katika sekta ya afya.

Vilevile inajukumu la kuratibu na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Mganga Mkuu wa Serikali kwenye masuala yote yanayohusiana na huduma za Afya kinga nchini, kuratibu usanifu, uendelezaji na usambazaji wa taarifa za Afya Kinga pamoja na nyenzo za mawasiliano nchini. ‎

You Might Also Like

TARURA yaimarisha ubora wa barabara kwa kuwa na maabara mikoani

Jeshi La Uhifadhi Wasisitizwa Kuzingatia Misingi ya Haki za Binadamu

Wamiliki Migodi Wapewa Siku 30 Kufanya Usajili

Makamanda Wa Polisi Msiende Nyumbani na Vyeo Vya Ukamanda

TTCL Yaweka Punguzo Kubwa Kwa Vifaa Vya Mobile Kwenye Sabasaba

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Miradi iliyokamilika ianze kutoa huduma- Nyamoga
Next Article Mauaji Yanayotokea Ni Aibu-Butiku
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

UDOM Yatafiti Dawa za Malaria, Vidonda vya Tumbo, Kisukari Kutoka Mimea ya Asili
Habari July 5, 2025
Wanafunzi UDOM Wavumbua Mafuta ya Asili Kutoka Mabaki ya Zabibu
Habari July 5, 2025
Taasisi Ya Confucius Imezindua Kitabu Cha Kujifunza
Habari July 5, 2025
PSPTB Yatangaza Usajili wa Mitihani ya 31 ya Kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi
Habari July 4, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?