MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Homa ya nyani mjadala wa dharura kwa mawaziri wa afya Afrika
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Homa ya nyani mjadala wa dharura kwa mawaziri wa afya Afrika
Habari

Homa ya nyani mjadala wa dharura kwa mawaziri wa afya Afrika

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu – Ethiopia
MAWAZIRI  wa Afya wa nchi za Afrika wanatarajiwa kukutana kwa dharura kabla ya mwisho wa mwezi Agosti kujadiliana, kupitisha  mikakati pamoja na kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nyani (Mpox) barani Afrika.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaalamu ya Mawaziri wa Umoja wa Afrika wanaosimamia Afya, Lishe, Idadi ya Watu na Udhibiti wa Dawa ametoa uamuzi huo wakati wa kufunga kikao cha Tano cha kamati mahususi ya kitaalam ya Mawaziri wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) Jijini Addis Ababa, Ethiopia.
“Nimefikia uamuzi huu baada ya kikao hiki kupokea taarifa ya Taasisi ya African (CDC) kuhusu hali ya ugonjwa wa Mpox barani Afrika ambapo ilielezwa kuwa takribani nchi Tisa za Afrika zina wagonjwa na hivyo kuwepo hatari ya ugonjwa kusambaa katika nchi nyingine za Afrika.” amesema Waziri Ummy
Amesema, taarifa ya African CDC ilionesha kuwa kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Julai, 2024 jumla ya watu 14,250 wameathirika na ugonjwa huo wa Mpox na kati ya hao watu 456 wamefariki.
Aidha, wakati wa kuhitimisha kikao hicho cha Tano cha kamati mahususi ya kitaalam ya Mawaziri wa Umoja wa Afrika (AU) wanaoshughulikia masuala ya Afya, lishe, Idadi ya watu na udhibiti dawa, Waziri Ummy amewapongeza washiriki wote wa kikao hicho.
 Pamoja na pongezi hizo Waziri Ummy amewaelekeza nchi wanachama kutekeleza masuala yote yaliyokubaliwa katika Kikao hicho yakiwemo ya kufanya maboresho ya kisera kwa nchi wanachama na kutekeleza mipango ya Kitaifa ya kudhibiti magonjwa ya kuambikiza na yasiyo ya kuambukiza.
“Pia, tuendelee kuimarisha huduma za Lishe na Afya ya akili hususani kwa vijana na udhibiti wa bidhaa tiba zisizokidhi viwango na dawa bandia, nchi wanachama zimetakiwa kuandaa Mpango wa kupambana na bidhaa tiba duni na bandia ambao utajumuisha udhibiti wa bidhaa tiba mipakani.” Amesema Waziri Ummy
Waziri Ummy amesisitiza uimarishaji wa mtandao wa maabara za bidhaa tiba za nchi wanachama na kupunguza uagizaji wa bidhaa tiba kutoka nje ya Bara la Afrika na kuhamasisha uzalishaji wa ndani pamoja na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu athari za bidhaa tiba duni na bandia pamoja na kuandaa mfumo wa ukusanyaji wa bidhaa tiba duni na bandia.
Tanzania ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia Agosti, 2024 hadi Agosti, 2026.

You Might Also Like

Waziri Mkuu Majaliwa Kuongoza Harambee Ya Mei Mosi Kitaifa

Mdemu Awataka Wafanyabiashara Ndogo Ndogo Kuchangamkia Mkopo

Masauni: Mapendekezo Ya Kulifanya NEMC Kuwa Mamlaka Yamepokelewa

Kumekucha Uzinduzi wa Washirika wa Tamasha, Tuzo Za Filamu Tanzania 2025

SUA Chatumia Ngamia Mafunzo Ya Vitendo Kwa Wanafunzi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TSB yaanzisha ‘special’ Mkonge BBT
Next Article Zifahamu hifadhi za bahari na maeneo tengefu.
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?