MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Hivi Ndivyo Vipaumbele Vya Maliasili
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Hivi Ndivyo Vipaumbele Vya Maliasili
Habari

Hivi Ndivyo Vipaumbele Vya Maliasili

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage.
WIZARA ya Maliasili na Utalii  imebainisha vipaumbele 10 ambavyo Wizara na taasisi zake zitatekeleza kwa mwaka 2025/26.
Akiwasilisha mpango wa mapato na matumizi kwa Wizara na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2025/26, Waziri wa Maliasili na Utalii ,Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara itatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maeneo ya vipaumbele 10.
Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kuendelea kutangaza utalii ndani na nje ya nchi kupitia matangazo katika ligi kuu za michezo mashuhuri duniani, mashindano ya kimataifa.
Pia kupitia mashirika ya ndege, misafara ya utangazaji utalii, matamasha makubwa ya kimataifa na mitandao mbalimbali ya kimataifa na vyombo vya habari.
Dkt. Chana amesema pia kuibua na kuendeleza mazao ya utalii ya kimkakati ikiwemo maeneo ya malikale pamoja na utalii wa fukwe, mikutano na matukio, meli, michezo, tiba na utamaduni.
Pia kuboresha miundombinu ya utalii na uhifadhi ikiwemo barabara, viwanja vya ndege na huduma za utalii.
Dkt. Chana amesema pia kuimarisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika usimamizi wa uhifadhi na rasilimali, ufuatiliaji, utangazaji na uendeshaji wa shughuli za utalii.
Pia kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori, misitu, nyuki na malikale na kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao ya misitu na nyuki.
Dkt. Chana amesema pia kuendelea kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa takwimu mbalimbali, kufanya tafiti za kimkakati na kutoa huduma za ushauri zinazohusu masuala ya uhifadhi endelevu wa wanyamapori, misitu na nyuki, malikale na uendelezaji utalii.
Amesema vipaumbele vingine ni pamoja na uelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za wanyamapori, malikale, misitu na ufugaji nyuki.
Pia kuimarisha usimamizi wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato yatokanayo na shughuli za utalii na uhifadhi.
Amesema pia kuandaa na kufanya Mapitio ya Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali ya kusimamia na kuendeleza Sekta ya Maliasili na Utalii.

You Might Also Like

Mwanjala Wa TRC Aelezea Umuhimu Wa VETA

Majukwaa YA Dini Yaimarishe Mapambano Dhidi ya Magonjwa Ya Mlipuko

Changamoto uchakataji Mkonge kupatiwa ufumbuzi

Miradi iliyokamilika ianze kutoa huduma- Nyamoga

NSSF Kutoa Mafao Siku Moja Baada ya Kustaafu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Watanzania Watakiwa Kufanya Kazi Kwa Bidii
Next Article JAB Yaanza Rasmi Kutoa Vitambulisho Kwa Waandishi Wa Habari
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

JAB Yaanza Rasmi Kutoa Vitambulisho Kwa Waandishi Wa Habari
Habari May 19, 2025
Watanzania Watakiwa Kufanya Kazi Kwa Bidii
Habari May 19, 2025
Tido Mhando: Marufuku Kuwasilisha Vyeti, Nyaraka Za Kughushi Maombi ya Ithibati, Press Card
Habari May 19, 2025
Shen Zhiying: Mkongwe Aliyeanzisha Kozi Ya Kiswahili Nchini China
Makala May 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?