MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt. Ndumbaro : Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Imefanikiwa 
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt. Ndumbaro : Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Imefanikiwa 
Habari

Dkt. Ndumbaro : Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Imefanikiwa 

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage.
DODOMA: JUMLA ya Mikoa 25 imefikiwa na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, toka kuzinduliwa kwake Aprili mwaka juzi 2023.
Waziri wa 0katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema hayo alipotoa taarifa kwa Waandishi wa Habari juu ya mafanikio ya Wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
 Amesema Ili kuhitimisha nchi nzima kwa upande wa Tanzania Bara, katika Mkoa wa Dar es Salaam kampeni hiyo itatekelezwa Juni, 2025.
Amesema upande wa Tanzania Zanzibar, utekelezaji wa Kampeni hiyo umefanyika katika mikoa mitatu na hivyo kukamilisha maeneo yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isipokuwa Dar es Salaam.
Amesema Kupitia Kampeni hiyo, jumla ya Halmashauri 180, Kata 1,907 na Vijiji/Mitaa 5,702 ilifikiw, na jumla ya wananchi  2,698,908  walifikiwa na kupata elimu na huduma za kisheria kupitia mikutano ya ana kwa ana.
Pia amesema  Idadi ya Mashirika yanayotoa Huduma za Msaada wa Kisheria yameongezeka kutoka 84 Novemba, 2021 hadi 377 mwaka 2025.
Vile vile idadi ya Wasaidizi wa Msaada wa kisheria imeongezeka kutoka 617 mwaka 2021 hadi 2,205 mwaka 2025.
Katika hatua nyingine amesema  Serikali imeanzisha madawati ya Msaada wa Kisheria katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 184.
Na jumla ya watumishi 449 wameajiriwa ili  kuwezesha  nadawati hayo kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
“Tangu kuanzishwa kwa madawati hayo, jumla ya wananchi 6,427,738  wamepatiwa elimu juu ya masuala ya kisheria na haki za binadamu.
“Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekamilisha uhakiki wa mwisho wa Sheria Kuu 300 kati ya 446 zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.
“Hii ni sehemu ya jitahada za Serikali  katika kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria na kuimarisha misingi ya utoaji haki.
“Serikali imeanzisha Kituo cha Huduma kwa Mteja ambapo mwananchi hupata fursa ya kuwasilisha malalamiko na hoja mbalimbali za kisheria moja kwa moja,” amesema.

You Might Also Like

Vijana Wahimizwa Kushiriki Kikamilifu Soko Huru la Afrika

Wajumbe TSC watakiwa kutembelea ofisi ngazi ya wilaya

Maandalizi Mei Mosi Yapamba Moto Singida

August 10, 2024

SADC Yasisitizwa Kuhusu Safari ya Ukombozi wa Kiuchumi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Senyamule Ahamasisha Ushiriki Wa Vijana Katika Uchaguzi
Next Article TDB Yaheshimisha Tasnia Ya Maziwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Apongeza Jeshi La Magereza Kurasimisha Ujuzi Kwa Wafungwa
Habari August 27, 2025
Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano
Habari August 27, 2025
Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini
Habari August 27, 2025
VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Habari August 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?