MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt. Mushongi: Mahindi Ni Nguzo Kuu ya Uchumi na Usalama wa Chakula
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt. Mushongi: Mahindi Ni Nguzo Kuu ya Uchumi na Usalama wa Chakula
Habari

Dkt. Mushongi: Mahindi Ni Nguzo Kuu ya Uchumi na Usalama wa Chakula

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
MOROGORO: TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), imesema kuwa tafiti zinazofanyika zimejikita kupunguza athari za visumbufu mbalimbali vikiwemo vya hali ya hewa  kama ukame, joto la kupita kiasi, rutuba hafifu, visumbufu vya kibaiolojia kama wadudu, magugu na magonjwa.
Mkurugenzi wa TARI Ilonga iliyopo Kilosa Morogoro,  ambaye pia ni Msimamizi wa Mahindi nchini, Dkt. Arnold Mushongi, amesema hayo katika Maonesho ya nanenane Kanda ya Mashariki.
Amesema TARI Ilonga imebuni teknolojia zinazoongeza uhimilivu wa uzalishaji katika mazingira changamoto, ili kuhakikisha kuwa mkulima anapata mavuno mengi kupitia mbegu bora na za kisasa.
Amesema Programu ya utafiti wa mahindi ni kubwa kuliko zote kutokana na umuhimu wa zao hilo, ambalo siyo tu ni chakula kikuu kwa Watanzania, bali pia ni zao la biashara linalotoa mchango mkubwa kwa taifa kupitia fedha za kigeni, viwanda, na ajira.
“Mahindi ni zao pana linalofanyiwa tafiti nyingi kutokana na matumizi yake mbalimbali.
“Hata hivyo, Tanzania bado haijalitendea kazi ipasavyo. Rais  Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa Tanzania inaweza kulisha Afrika, na mahindi ni zao kuu katika kufanikisha azma hiyo,” amesema.
Amesema mahindi mengi ya ziada yanauzwa nje ya nchi kutokana na kuwepo kwa soko kubwa. Uwezo wa taifa kuzalisha mahindi ni tani milioni 18 kwa mwaka, lakini bado tupo kwenye theluthi moja ya kiwango hicho.
Amesema Kitafiti, maeneo ya uzalishaji yamegawanywa katika uwanda wa joto, uwanda wa kati na uwanda wa juu kwa ajili ya kufanya tafiti sahihi kulingana na mazingira.
Changamoto nyingine kubwa ni upotevu baada ya mavuno licha ya kuzalisha tani milioni saba kwa mwaka.
Kwa miaka mingi, juhudi zimekuwa zikielekezwa kwenye kuongeza uzalishaji, lakini sasa tunasisitiza pia kulinda ubora wa mazao baada ya kuvunwa.
Dkt. Mushongi anasisitiza kuwa serikali iwekeze zaidi kwenye tafiti zinazolenga kupunguza pengo hilo, ili kuhakikisha kuwa kinachozalishwa kinabaki na ubora unaokusudiwa hadi sokoni.

You Might Also Like

Dodoma Yang’ara Katika Mfumo wa Stakabadhi Ghalani

Bonifas Jacob aahidi  akishinda Uenyekiti Kanda ya Pwani hatakaa ofisini

VETA: Miaka 30 ya Kuinua Ujuzi na Kuunda Wataalamu wa Kesho

TPHPA Yapata Dawa Ya Visumbufu Vya Mazao

Wanafunzi Waliokwenda China Watakiwa Kuiwakilisha Tanzania Vizuri

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yawekeza Katika Utafiti wa Alizeti, Wakulima Wapate Mbegu Bora
Next Article Dodoma Yazizima Wakati Samia, Nchimbi  Wakichukua Fomu Ya Urais
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Madaktari Kutoka Ireland Watoa Matibabu Ya Mifupa Kwa Watoto MOI
Habari October 20, 2025
Mwalim: Nikichaguliwa urais, Kigaila atakuwa Waziri Mkuu wangu
Habari October 20, 2025
ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?