MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: DKT. Biteko Azindua Mradi Utakaowakwamua Vijana Kiuchumi Katika Maeneo Yanayopitiwa Na Bomba La Mafuta Ghafi  (EACOP)
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > DKT. Biteko Azindua Mradi Utakaowakwamua Vijana Kiuchumi Katika Maeneo Yanayopitiwa Na Bomba La Mafuta Ghafi  (EACOP)
Habari

DKT. Biteko Azindua Mradi Utakaowakwamua Vijana Kiuchumi Katika Maeneo Yanayopitiwa Na Bomba La Mafuta Ghafi  (EACOP)

Author
By Author
Share
8 Min Read
Na Mwandishi Wetu
NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati  Dkt. Doto Biteko leo amezindua  Mpango wa Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Vijana (YEE) ambao unagusa maeneo yanayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ikiwa ni jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kuhakikisha kuwa jamii zilizo karibu na miradi zinanufaika na miradi hiyo.
Akizindua mradi huo katika  Kijiji cha Bukombe, wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita  Dkt. Biteko amesema mradi huo wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi ni moja ya miradi iliyopangwa kuwezeshwa na Kampuni ya EACOP kwa kipindi cha ujenzi na baada ya ujenzi ikiwa ni sehemu ya Uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii.
Amesema mradi huo umepangwa  kuwafikia zaidi ya vijana 12,261 ambapo miongoni mwao wanawake ni 6,130; wanaume 4,905 na makundi maalumu ni 1,226 katika awamu ya kwanza inayohusisha Mikoa ya Geita, Kagera, Tabora na Tanga.
” Tunapozindua mradi huu hatuna budi kuwashukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda.
Viongozi wetu hawa kwa nia yao  ya dhati na moyo wa uzalendo wameuendeleza na  kuusimamia kikamilifu mradi huu wa EACOP ambao umefikia asilimia 65, tumefikia hapa sababu ya msukumo wao wa kutekeleza mradi huu ” Amesema Dkt. Biteko
Ameeleza kuwa  tangu kuanza kwa mradi wa EACOP  mwaka 2022 hadi sasa,  jumla ya Watanzania 9,194 wamepata nafasi za kufanya kazi ndani ya mradi na hivyo kuwa fursa kwao ya kujipatia kipato, mwaka 2024 kampuni ilitoa mafunzo maalumu kwa Vijana 170 na kuwapatia kazi kwenye mradi, Vijana wengine 110 wapo katika masomo na wanatarajiwa kujumlishwa  pia katika Mradi huo pamoja na kutoa
ufadhili wa Vijana 238 katika vyuo mbalimbali nchini.
Habari Picha 9043
Amesema wananchi wanaopitiwa na miradi wanayo haki ya kunufaika na miradi lakini wana wajibu wa kulinda miundombinu ya mradi na kuufanya kuwa ni sehemu yao kwani unachangia pia kubadilisha maisha ya wananchi.
 Pia, Dkt. Biteko ameipongeza kampuni ya EACOP  na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC) kwa kusimamia kwa ufanisi mradi huo huku akisisitiza kuwa, ili wananchi waone mradi huo ni sehemu yao lazima waone faida zake  hivyo miradi kama ya YEE inawapa chachu wananchi kulinda miundombinu ya EACOP kwa  wivu mkubwa.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, kampuni mbalimbali zinazotekeleza miradi kuhakikisha kuwa hawaweki mkazo  kwenye kuongeza ujuzi tu kwa wananchi bali wanawapatia mitaji ili waweze kufanya vizuri zaidi.
Aidha, amewaasa vijana kuchangamkia fursa zinazotokea kwenye miradi, wajitume, wawe waaminifu pale wanapopata fursa na kueleza kuwa Serikali itaendelea kuwatengenezea fursa  ili wajikwamue kiuchumi na kuleta maendeleo nchini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira),  Patrobas Katambi amesema Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengeneza mipango mikakati ya kuhakikisha vijana wanapewa fursa za ajira na mitaji kwenye maeneo mbalimbali ambapo mpango wa YEE ni kielelezo cha matokeo ya mipango hiyo.
Ameeleza kuwa, kumekuwa na programu mbalimbali ikiwemo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo kupitia programu hiyo zaidi ya shilingi trilioni tatu zilitolewa kwa Watanzania  takriban milioni 24 ikiwemo Wanawake,  Vijana na Makundi maalum kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi
Mkuu wa Mkoa Geita, Martine Shigella akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa inayopitiwa na mradi wa EACOP amesema kuwa mradi wa EACOP ni miongoni mwa miradi mikubwa ambayo wananchi wa Geita wamenufaika nayo kwa namna mbalimbali ikiwemo ajira za moja kwa moja na muda na mfupi pamoja na  mnyororo wa thamani kupitia biashara ya vyakula, mbogamboga, matunda.
Amesema Mpango wa  uwezeshaji wa vijana kiuchumi ni matunda ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameendelea kuhakikisha vijana wanapata elimu na ujuzi hivyo mpango wa YEE unaongeza chachu hiyo ya utoaji elimu na ujuzi kwa wananchi wakiwemo vijana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema utekelezaji wa mradi wa EACOP wenye urefu wa km 1443 ni moja ya miradi 17 inayotekelezwa na Wizara ya Nishati ikiwemo mradi wa Julius Nyerere ( MW 2,115) ambao umekamilika, miradi ya umeme ya Ruhudji,  Rumakali na Malagarasi pamoja miradi mingine ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia ukiwemo wa Eyasi Wembere.
Katika mradi wa EACOP amesema Serikali imechangia sh trilioni 1.12  ambazo ni hisa za Tanzania na kuna kampuni za kitanzania 200 ambazo zinafanya kazi mbalimbali katika mradi ambazo zitalipwa jumla ya shilingi trilioni 1.325 ikiwa ni moja ya matunda ya uwepo wa mradi huo nchini.
Akieleza sababu za kufanyika.kwa uzinduzi wa mradi wa YEE wiiayani Bukombe amesema kuwa Bukombe  kuna  kituo kikubwa zaidi cha kusukuma mafuta yatakayotoka nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga,   kuna kambi kubwa ya mradi wa EACOP na pia kilometa 20 za bomba hilo la mafuta zinapita katika eneo la Bukombe.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), Mussa Makame  ameeleza kuwa, TPDC imeendelea kushirikiana na kampuni ya EACOP kuhakikisha kuwa mahitaji ya wananchi yanabainishwa na kuzingatiwa katika utekelezaji wa mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Ameeleza kuwa mahitaji yaliyoainishwa katika mradi wa YEE yaliandaliwa kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa kwa ngazi ya vijiji, Kata na Halmashauri zilizopo maeneo linapopita bomba la mafuta.
Awali  Clare Haule – Meneja wa Uwekezaji na Uwajibikaji kwa Jamii katika kampuni ya EACOP amesema mradi wa YEE umeanzishwa kwa kutambua kwamba zaidi ya asilimia 65 ya idadi ya watu wa Tanzania ni vijana chini ya umri wa miaka 35. Hata hivyo, vijana wengi hasa katika maeneo ya vijijini wanakumbana na vikwazo vingi kama vile ukosefu wa ajira, ukosefu wa mafunzo ya ufundi stadi , na ugumu wa kupata mitaji ya kuanzisha au kukuza biashara.
Amesema awamu ya kwanza ya Mradi wa YEE  utawawezesha kiuchumi vijana katika mikoa ya Geita, Kgera,Tabora, na Tanga na  mikoa inayobaki itanufaika katika awamu ya pili ambayo ni Singida, Shinyanga, Dodoma na Manyara ambapo vijana watapewa ujuzi  unaolingana na mahitaji ya soko, kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha, na kuondoa vikwazo vya ujasiriamali na ajira binafsi.
Ameongeza kuwa, Mradi wa YEE ni sehemu ya Sera ya Uendelevu ya EACOP, chini ya nguzo ya Vizazi Vijavyo, inayolenga kujenga uwezo wa vijana na kuongeza upatikanaji wa fursa za kiuchumi katika jamii zinazoguswa na mradi.

You Might Also Like

Stamico Yapewa Tuzo Na FDH Kujali Wenye Ulemavu

Vijana 26 Kwenda Kujifunza Mafunzo Ya Vitendo Nje Ya Nchi

TARURA yaokoa kiasi kikubwa cha fedha kwa kujenga madaraja ya mawe

August 10, 2024

Mongella Atoa Maagizo Maalum Kwa Viongozi CCM

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article REA Kusambaza Majiko Banifu 10,650 Mkoa Wa Pwani
Next Article REA Yajivunia Mafaniko ya usambazji wa Teknolojia za Nishati Safi kwa Wananchi Vijijini
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Apongeza Jeshi La Magereza Kurasimisha Ujuzi Kwa Wafungwa
Habari August 27, 2025
Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano
Habari August 27, 2025
Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini
Habari August 27, 2025
VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Habari August 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?