Na Lucy Lyatuu
TAASISI Ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) imesema inatoa kozi ya namna ya kuchakata ngozi kuanzia mnyama anapochinjwa na pia inafundisha vijana na Wajasiriamali kutengeneza bidhaa za ngozi.
Mkufunzi Wa DIT kampasi ya Mwanza Sharif Mwangi amesema hayo wakati akizungumza katika Banda la DIT lililoko katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimaraifa maarufu kama sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam.
Amesema kozi hiyo ni mpya ambapo mwanafumzi atasoma kwa miaka mitatu ikilenga kutoa elimu ya namna ya kuchakata ngozi pamoja na kutengeneza bidhaa za ngozi ikiwemo mikoba,, mipira na hata viatu.
“Pia tunatoa huduma kwa Wajasiriamali ambapo wakileta ngozi sisi TaasisiI huzichukua na kuzichakata na kuwarudishia Ili waweze kutengeneza bidhaa tofautitofauti,” amesema Mwangi.
Ameongeza kuwa pia DIT hutoa elimu ya kiwango Cha shadada kwenye ngazi mbalimbali na kwamba ziko kozi 17 za nyanja tofautitofauti zikiwemo zile zinazohusu Teknolojia.
“Ni kozi ya miaka kitati na mwanafumzi aliyepata alama ya D katika masomonya Hesabu,Fizikia, kemia na baiolojia ndio wahusika wakuu,”amesema Mwangi.
Amesema ngozi wanazotumia katika kutoa Mafunzo ni za wanyama kama ngombe,mbuzi lakini pia wakitumia nyara kama nyoka lakini wakiwa na Kibali maalum..