Na Lucy Ngowi
CHAMA cha Kikomunisti cha China (CPC), kimesema chama hicho na serikali yake kinatambua juhudi kubwa za kuleta maendeleo zinazofanywa na Rais Samia
Suluhu Hassan nchini Tanzania.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Idara ya Mambo ya Nje wa CPC, Liu Jianchao alipokutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, katika Makao Makuu ya Ofisi za Idara ya Mambo ya Nje ya CPC, Jijini Beijing China leo.
Jianchao amesema kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia, Tanzania imekuwa na
mabadiliko makubwa, yanayoonekana katika nyanja zote za viashiria vya ukuaji uchumi.
Balozi Nchimbi, pamoja na
Kufikisha salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Samia, amesema kuwa CCM, Serikali zake mbili na Tanzania kwa ujumla wanaichukulia China, ni mojawapo ya mifano ya kuigwa.

Dkt. Nchimbi amesema chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping, CPC imeweza kuiongoza China kupiga hatua za maendeleo makubwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.
“Kupitia mazungumzo hayo, Balozi Nchimbi na Jianchao, wamerejea msingi imara wa
uhusiano wa vyama vyao na nchi hizi mbili, tangu wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong,

.
“Wamekubaliana umuhimu wa
kuendelea kuimarisha udugu huo wa kirafiki, kwa ajili ya manufaa ya Tanzania na China,” imesema taarifa iliyotolewa na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Rabia Hamid.

Taarifa hiyo imesema Mkutano huo wa
Balozi Nchimbi na Jianchao ni sehemu ya ratiba ya ziara ya Ujumbe wa Viongozi wa CCM nchini China, iliyoanza Agosti 24, 2024, inayolenga kuendeleza na
kuimarisha zaidi urafiki wa kihistoria kati ya vyama vya CCM na CPC na uhusiano wa
kidiplomasia kati ya Tanzania na China, ambao umedumu kwa miongo sita sasa.