Na Waandishi Wetu
BAADA ya Rais wa Marekani Donald Trump kuingia madarakani, alifunga Shirika la Maendeleo la Marekani (MCC), April 23, 2025.
Theluthi mbili ya misaada ya Marekani ilikuwa ikitolewa kwa nchi za Afrika, kufadhili barabara, umeme na umwagiliaji. Hivyo kujiondoa kwake kunaacha miradi ambayo haijakamilika na kudhoofisha uchumi wa nchi hizo.
Aprili 24 mwaka huu, 2025 Shirika la Habari la France (AFP), liliripoti kwamba utawala wa Rais Trump uliamuru shirika hilo, Aprili 23 ambalo lilianzishwa mwaka 2004 kwa kuungwa mkono na Chama cha Democratic na Chama cha Republican.
Shirika hilo limefanya uwekezaji mkubwa katika miradi ya miundombinu Barani Afrika, na katika nchi nyingine zinazoendelea.
Mtaji wake wa uwekezaji katika Bara la Afrika ni takribani dola bilioni 10, huku miradi mingi ikiwa mbioni kujengwa.
Rais Donald Trump alitia saini agizo la utendaji katika ofisi ya Ikulu ya White House, Jumatano, Aprili 23, 2025
Mnamo Aprili 23 mwaka huu, watendaji wa shirika hilo walitangaza katika mkutano wa wafanyakazi kwamba shirika hilo linafungwa kwa utaratibu, na miradi yote itasimamishwa.
Pia taarifa za ndani zilionyesha kwamba Idara ya Ufanisi ya Serikali ya Marekani inayoongozwa na Elon Musk, ililitaka shirika hilo kupunguza idadi ya wafanyakazi kwa kiasi kikubwa.
Hivyo Kama hakuna mshirika mwingine kuchukua nafasi yake, miradi inayoendelea kama mradi wa uboreshaji wa mtandao wa usafiri wa Niger, mradi wa ujenzi wa mfumo wa kusambaza umeme wa Nepal na mradi wa umwagiliaji wa kilimo wa Msumbiji inakabiliwa na hatari ya kusitishwa.
Rais Trump anapinga kutoa misaada ya kimaendeleo, kwa sababu anaamini hainufaishi Marekani moja kwa moja.
Awali Trump alikuwa amefunga Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Kufungwa kwa Shirika hilo la MCC kumefichua zaidi fikra zake za ‘biashara kwanza’, kwani wadadisi wa mambo wanaona kama anaangalia faida zaidi.
Hivyo anaona kwamba utoaji wa misaada ni upotezaji wa rasilimali.
Uamuzi huo umesababisha madhara makubwa pia usitishwaji wa miradi ya maendeleo katika nchi nyingi zinazoendelea.
Katika kipindi muhimu ambacho utaratibu wa kimataifa unarekebishwa upya, Marekani ingeweza kuimarisha uvutano wake wa mfumo wa kisiasa kwa kupitia misaada ya kimataifa.
Bila shaka, uamuzi wa Rais Trump ni usaliti wa ushirikiano wa kimataifa na kanuni za kimataifa, ambao unaweza kuchafua vibaya sifa za Magharibi katika nchi zinazoendelea.
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wamesema kuwa Rais Trump “anafidia nakisi ya bajeti ya Marekani kwa kuharibu utaratibu wa kimataifa”.
Ikilinganishwa na Marekani, China siku zote imekuwa ikitekeleza kikamilifu ujenzi wa Jumuiya ya Ngazi ya Juu ya China – Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja. Kupitia Mpango wa ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ (BRI) na ushirikiano wa ujenzi wa miundombinu na mengineyo.
Hivyo China inaendelea kusukuma mbele maendeleo ya nchi za Afrika.
Utekelezaji wa miradi kama Reli ya Kisasa ya Mombasa-Nairobi (SGR) na Daraja la J.P. Magufuli nchini Tanzania umedhihirisha azma thabiti ya China na Afrika ya kufanya kazi pamoja kwa ajili ya maendeleo na kunufaishana,
Pia umethibitisha kwamba ushirikiano kati ya China na Afrika umekuwa mfano bora kwa ushirikiano wa kimaendeleo duniani.
Mwandishi Ning Yi, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).
Barua pepe:02706@shisu.edu.cn
Mwandishi Ye Tianfa, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Tianjin (TFSU)
Barua pepe: tianfa202123@163.com
JibuSambaza |