– Dar es Salaam Ni Salama Kuelekea Uchaguzi Mkuu
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM,: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema ujenzi wa daraja la Jangwani umeanza.
Chalamila amesema hayo alipozungumza na Waandishi wa Habari mkoani Dar es Salaam leo Aprili 18, 2025.
Amesema ujenzi huo umeanza kwa sababu Mkandarasi ameanza ujenzi wa karakana ya kuhifadhia vifaa.
” Katika kuboresha miundombinu Serikali mkoani Dar es Salaam imeanza ujenzi wa daraja la Jangwani, wananchi msiwe na shaka juu ya ujenzi huo ambao unakwenda kuwa suluhisho la mafuriko eneo hilo,” amesema.
Katika kikao hicho na wana Habari pia amezungumzia usalama wa Mkoa, jumbe zinazozagaa juu ya mafuriko na hatua zinazochukuliwa na Serikali, Kasi ya ulipaji kodi, maboresho ya miundombinu ya barabara pamoja na nafasi ya mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.
Amezungumzia pia mpango wa ujenzi wa barabara katika Mkoa huo kupitia Mradi wa DMDP ambapo amesema wakandarasi wengi wameshaingia kazini.
Pia amewahakikishia wananchi
barabara ambazo bado ujenzi haujaanza ndani ya muda mfupi kazi itaanza,
Vile vile amesisitiza juu ya mpango wa serikali kuimarisha usafiri wa mwendokasi kupitia wawekezaji binafsi.
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu, amesema licha ya tofauti za itikadi za kisiasa zilizopo, Mkoa utaendelea kuwa salama kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Kuhusu Mpango wa Biashara saa 24, amesema uwepo wa bandari, uwanja wa ndege wa kimataifa,kituo cha Mabasi cha Magufuli, umeme na soko la kimataifa la Kariakoo ni nyenzo muhimu kufikia lengo la biashara saa 24
Chalamila amewatakia Kheri ya Pasaka wakristo wote na wakazi wa Dar es Salaam kwa ujumla kusherekea kwa Amani na Utulivu