DAR ES SALAAM: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema wagombea takribani 500,000 walijitokeza katika mchakato wa kura za maoni katika nafasi mbalimbali nchi nzima kwenye uchaguzi wa Serikali Za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.
Aidha wana CCM waliojitokeza kujiandikisha kwa nchi nzima ni zaidi ya milioni 10, hali inayodhihirisha kuwa chama hicho kinaongoza ikilinganishwa na vyama vingine.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema hayo leo Mkoani Dar es Salaam, huku akiwapangeza wana CCM kwa ushiriki huo.
Amesema Chama kimefurahishwa na hamasa iliyokuwepo kwa wanachma wake kwani imevunja rekodi kwa chaguzi zote zilizofanyika.
Amesema kwa hamasa hiyo CCM imethibitisha ndio chama kikubwa Afrika na Tanzania.