MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima
Habari

Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA:  MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imeendelea kutoa elimu kuhusu njia bora, salama na rafiki kwa mazingira za kudhibiti visumbufu vya mazao.
Mojawapo ya njia hizo ni matumizi ya ndege wa aina ya bundi kwa ajili ya kudhibiti panya mashambani.
Ofisa Kilimo kutoka TPHPA, Mathias Bernard ametoa elimu hiyo katika Maonesho ya Nanenane ya Kitaifa na Kimataifa yanayoendelea mkoani Dodoma.
Amesema jitihada zote hizo zinafanywa na TPHPA kuhakikisha wakulima wanapata mazao bora kwa tija,
Amesema katika maonesho hayo, TPHPA  imekwenda na suluhisho la kipekee ambalo linatumia teknolojia ya asili katika kukabiliana na changamoto sugu ya panya kwenye mashamba ya wakulima wadogo na wa kati.
Amesema Kituo cha Kudhibiti Baa la Panya Morogoro ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa kudhibiti viumbe waharibifu wa mazao kama panya na jamii zake, ambao husababisha hasara kubwa kila mwaka kwa wakulima nchini.
“Lengo letu katika kushiriki maonesho haya ni kuwaelimisha wananchi kuhusu aina mbalimbali za panya wanaopatikana katika mazingira yao, madhara wanayosababisha na njia mbalimbali za kisasa na za asili za kuwadhibiti,” alisema Bernard.
Amesema kwa muda mrefu wakulima wamekuwa wakitegemea sumu na mitego ya kawaida, lakini sasa TPHPA inahamasisha matumizi ya mbinu za kibaiolojia, ikiwemo kutumia ndege aina ya bundi, ambao ni maadui wa asili wa panya.
Amesema  bundi ni ndege anayewinda usiku, na chakula chake kikuu ni panya.
“Tunashauri wakulima watengeneze viota vya bundi na kuviweka kwenye miti inayopakana na mashamba yao. Hii huwavutia bundi kuja kutaga na kuishi humo. Watoto wa bundi wakikua, huanza kutoka usiku kutafuta chakula na chakula chao ni panya,” amesema.
Amesema kwa wastani, bundi mmoja anaweza kula panya wasiopungua watatu kwa siku.
Amesema mbinu hiyo siyo tu inapunguza gharama za kudhibiti visumbufu, bali pia inalinda afya ya binadamu, ardhi, na mazingira dhidi ya madhara ya sumu kali ambazo mara nyingi hutumika bila tahadhari.
Amewashauri wakulima nchini kuanza kutumia njia hiyo ya asili kama sehemu ya mikakati ya kudumu ya kudhibiti panya.
Amesema kuwa mbali na bundi, kuna njia nyingine za kibaiolojia na kimazingira zinazofaa kutumiwa sambamba ili kupata matokeo bora.
“Kwa kutumia bundi, wakulima wanapunguza matumizi ya sumu, wanatunza mazingira, na kuongeza tija ya uzalishaji. Hii ni teknolojia rafiki kwa kila mkulima,” amesema.

You Might Also Like

TUCTA Yaanza Maandalizi Ya Mei Mosi

NEMC Kupambana Na Magugu Maji Ziwa Victoria

UDSM Yaja Na Bajaji Inayotumia Maji Na Mafuta

Rais Samia Afungua Barabara Ya Mbinga-Mbamba Bay Yenye Km 66-Ruvuma

PIC Uwekezaji Bidhaa Za Ngozi Utaongeza Mapato

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ofisa wa TARI Kuwapo Kila Kituo cha Umwagiliaji – Naibu Katibu Mkuu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ofisa wa TARI Kuwapo Kila Kituo cha Umwagiliaji – Naibu Katibu Mkuu
Habari August 6, 2025
Mbinu Mpya za Kilimo kwa Vijana Zapata Umaarufu Nanenane Banda La VETA
Habari August 6, 2025
VETA Yatahadharisha Changamoto ya Kuzidisha Uchanganyaji wa Chakula Cha Mifugo
Habari August 6, 2025
UDSM Yaanzisha Mkakati Kuokoa Nyuki Wadogo
Habari August 6, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?