MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Biashara Kati Ya Tanzania Na Uturuki Yapanuka Kwa Kiasi  Kikubwa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Biashara Kati Ya Tanzania Na Uturuki Yapanuka Kwa Kiasi  Kikubwa
Habari

Biashara Kati Ya Tanzania Na Uturuki Yapanuka Kwa Kiasi  Kikubwa

Author
By Author
Share
3 Min Read

 

Na Lucy Lyatuu

BIASHARA kati ya Tanzania na Uturuki katika muongo mmoja uliopita, imepanuka kwa kiasi kikubwa kwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 284  kwa mwaka 2024 ambapo kiwango cha  thamani ya dola milioni 217 ni usafirishaji bidhaa kutoka Uturuki.

Makamu wa Rais Biashara wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Boniphace Ndengo amesema hayo Dar es Salaam wakati akizindua jukwaa la mazungumzo ya kibiashara (B2B) baina ya Tanzania na Uturuki.

Tayari Ujumbe wa wafanyabiashara 36 kutoka  kampuni 16 za Kituruki yapo nchini Tanzania  kushirikiana kwa karibu na wawakilishi wa sekta ya chuma ya Tanzania ,  kwa lengo la kupanua wigo wa masoko nje ya nchi.

Habari Picha 9253

Katika muktadha huo, Chama cha Wauzaji wa Chuma wa Uturuki (CiB) wako nchini kuanzia septemba 2-6,2025  kujadili fursa mbalimbali za chuma, kujenga ubia wa wauzaji, kuwa na mipangilio ya usambazaji, na uwekezaji katika vifaa vya uzalishaji kutumia chuma.

Akizungumza, Ndengo amesema  mkusanyiko huo sio tu kikao cha mtandao-ni jukwaa ambalo mawazo hukutana na fursa, na ambapo maono ya pamoja ya ukuaji yanapata kujieleza kwa vitendo.

Habari Picha 9254

“Tanzania na Uturuki wanafurahia urafiki unaojengwa katika kuheshimiana, mshikamano na kukuza ushirikiano wa kiuchumi,” amesema Ndengo na kuongeza  kuwa katika muongo mmoja uliopita, nchi hizo  mbili biashara imepanuka kwa kiasi kikubwa.

Amesema Uturuki inatambulika kimataifa kwa uvumbuzi na ubora wake katika uzalishaji wa chuma, wakati Tanzania inakabiliwa na ukuaji wa haraka wa viwanda na upanuzi wa miundombinu.

Amesema ushirikiano  huo hautaimarisha tu minyororo ya thamani lakini pia kutengeneza ajira na kuhamisha teknolojia hadi Tanzania.

“Chuma bado ni uti wa mgongo wa maendeleo ya viwanda-kusaidia ujenzi, nishati,usafiri, na viwanda. Mahitaji ya

Habari Picha 9255

Tanzania ya bidhaa bora za chuma yanaendelea kuongezeka kulingana na miradi mikubwa inayoendelea.

Makamu Mwenyekiti wa ujumbe huo, Ugur Dalbeler amesema uchumi unaokuwa wan chi hiyo unatoa fursa kubwa za  ushirikiano na mauzo kwa wauzaji wa Uturuki.

Amesema Tanzania ni  miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi katika Jangwala Kusini mwa Afrika na kwamba Uturuki inaendelea kuuza bidhaa zenye thamani yad ola  milioni 216 kwenda Tanzania na uwezo unaendelea kuongezeka.

 

Amesema katika sekta ya chuma wanasafirisha tani 40,000 mwaka 2024 na tani 19,400 katika miezi saba ya mwanzo yam waka huu,  jumla ya mauzo ya Tanzania ya bidhaa zilizoingizwa inaendelea kufikia dola bilioni 16.6.

Balozi wa Uturuki nchini,  Dk Bekir Gezer amesema Uturuki inaahidi kuendeleza biashara na kuwa bora kwa kuwa Tanzania  ni eneo bora kwa uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Habari Picha 9256

 

You Might Also Like

Mdau wa Maendeleo Goryo Ashinda Tuzo Ya Mlipa Kodi Bora

Watafiti, Wabunifu Waendelezwe Wasivunjwe Moyo- Biteko

Johari Ataka Ufasili wa Sheria za Uchaguzi Ukamilike

Homa ya nyani mjadala wa dharura kwa mawaziri wa afya Afrika

Wanafunzi Kutoka Veta Kushiriki Mafunzo Japan

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Polisi Dar Wakamata Magari 15  Yasiyo na Usajili Rasmi
Next Article Kasulu Yaandaa Bonanza La Michezo Kuhamasisha Uchaguzi Mkuu, Mapokezi Ya Mwenge
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CHAUMMA Kuunda Mamlaka ya Mazao ya Kimkakati – Salum Mwalim
Habari September 14, 2025
Heshima ya Udaktari Ni Mwito wa Kulitumikia Taifa: Dkt Ikomba
Habari September 14, 2025
Rais Wa CWT Suleiman Ikomba Sasa Ni Daktari
Habari September 13, 2025
Salum Mwalim: Nitarejesha Hadhi ya Kanda ya Ziwa na Kuinua Zao la Pamba
Habari September 12, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?