MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: NIC Yatoa Elimu ya Bima Kwenye Kijiji cha Bima, Maonesho ya Madini Geita
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > NIC Yatoa Elimu ya Bima Kwenye Kijiji cha Bima, Maonesho ya Madini Geita
Habari

NIC Yatoa Elimu ya Bima Kwenye Kijiji cha Bima, Maonesho ya Madini Geita

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
GEITA: SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) linaendelea kutoa elimu na huduma mbalimbali za bima kwa wananchi kupitia Kijiji cha Bima, kilichopo katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.
Ofisa Uhusiano Ephrasia Mawala amesema hayo katika maonesho ya madini mkoani Geita.
“Ushiriki wetu katika Kijiji cha Bima ni sehemu ya dhamira ya NIC ya kufikisha elimu ya bima kwa wananchi kwa njia rahisi na ya moja kwa moja, kwa kushirikiana na mamlaka na taasisi nyingine za sekta hii,” amesema.
Amesema maonesho hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kutoa elimu ya kifedha kwa wananchi, hasa kuhusu bima kama nyenzo ya kujikinga na athari za kiuchumi zinazotokana na majanga mbalimbali kama moto, ajali, maafa ya asili na mengineyo.
Amewakaribisha wananchi kutembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) katika Kijiji cha Bima, ili kupata huduma na maelezo kutoka kwa NIC pamoja na watoa huduma wengine wa bima waliopo katika eneo hilo.
Amesema Kijiji cha Bima ni mkusanyiko wa watoa huduma za bima kutoka kampuni mbalimbali nchini, unaoratibiwa na TIRA kwa lengo la kuwawezesha wananchi na wadau wa sekta ya madini na biashara kupata elimu, ushauri na huduma za bima kwa karibu.
Amesema NIC ikiwa ni shirika la umma linalotoa huduma za bima nchini, inashiriki kikamilifu kwa kutoa huduma za bima ya maisha, bima ya mali, bima kwa wachimbaji, pamoja na ushauri wa kitaalamu kuhusu aina sahihi za bima kulingana na mazingira ya kijamii na kibiashara.

You Might Also Like

Mfanyakazi Ana Wajibu Kupeleka Taarifa za Madai

Wafanyakazi waitwa kupeleka changamoto za kikazi CMA

Muhimbili yarejesha tabasamu kwa Karume baada ya miaka 25 ya mateso

Ridhiwani Ateta na Viongozi wa Vijiji Lugoba, Chalinze 

Vyombo vya Habari ni Kama Maji’ -Biteko 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article NIC Yaimarisha Uhusiano na Wateja Maonesho ya Teknolojia ya Madini Geita
Next Article Mwenyekiti TCCIA Geita Gabriel Ahamasisha Watanzania Kutumia Bidhaa Za Ndani
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe
Habari October 17, 2025
Mgombea NCCR-Mageuzi Awaasa Watanzania Wasikubali Propaganda
Habari October 17, 2025
Profesa Nombo: Ushirikiano wa VETA, Sekta Binafsi Waimarisha Mafunzo ya Ufundi Stadi
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?