Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 7, 2026
Habari Lucy Ngowi 6

Fema Mining & Drilling Mfano wa Kuigwa – Musukuma

Na Lucy Ngowi
GEITA: MBUNGE mstaafu anayegombea tena kiti cha Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Musukuma, amesema kuwa kampuni ya uchimbaji madini ya Fema Mining & Drilling ni mfano mzuri wa kuigwa.
Musukuma amesema hayo alipotembelea banda la Fema katika maonesho ya nane ya madini yanayoendelea mkoani Geita.
Habari Picha 9543
“Fema ni Watanzania, wanachimba kwenye mgodi wa Buckreef  . Walianza kama kiwanja cha Mpira, mwaka uliofuata wakajenga jengo la utawala. Sasa tunaendelea kusonga mbele na watu,” amesema Musukuma.
Amesema Fema Mining & Drilling ni kampuni ya Kitanzania inayomilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania. Inafanya shughuli zake za uchimbaji, ulipuaji, na uchorongaji katika mgodi wa Buckreef.
Habari Picha 9544
Ofisa Usalama wa kampuni hiyo, Victor Mkono amesema Fema imejidhatiti kusaidia jamii inayowazunguka katika nyanja mbalimbali.
Miongoni mwa michango hiyo ni pamoja na kuchimba visima vya maji safi na salama, kuchangia kuendeleza miradi ya shule, kusaidia vifaa vya hospitali, na kushiriki maonyesho mara kwa mara.
Aidha, halmashauri inanufaika na mapato ya Uwajibikaji wa Makampuni kutoka Fema Mining & Drilling kati ya shilingi milioni 159 hadi 400.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.