Na Lucy Lyatuu
BIASHARA kati ya Tanzania na Uturuki katika muongo mmoja uliopita, imepanuka kwa kiasi kikubwa kwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 284 kwa mwaka 2024 ambapo kiwango cha thamani ya dola milioni 217 ni usafirishaji bidhaa kutoka Uturuki.
Makamu wa Rais Biashara wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Boniphace Ndengo amesema hayo Dar es Salaam wakati akizindua jukwaa la mazungumzo ya kibiashara (B2B) baina ya Tanzania na Uturuki.
Tayari Ujumbe wa wafanyabiashara 36 kutoka kampuni 16 za Kituruki yapo nchini Tanzania kushirikiana kwa karibu na wawakilishi wa sekta ya chuma ya Tanzania , kwa lengo la kupanua wigo wa masoko nje ya nchi.

Katika muktadha huo, Chama cha Wauzaji wa Chuma wa Uturuki (CiB) wako nchini kuanzia septemba 2-6,2025 kujadili fursa mbalimbali za chuma, kujenga ubia wa wauzaji, kuwa na mipangilio ya usambazaji, na uwekezaji katika vifaa vya uzalishaji kutumia chuma.
Akizungumza, Ndengo amesema mkusanyiko huo sio tu kikao cha mtandao-ni jukwaa ambalo mawazo hukutana na fursa, na ambapo maono ya pamoja ya ukuaji yanapata kujieleza kwa vitendo.

“Tanzania na Uturuki wanafurahia urafiki unaojengwa katika kuheshimiana, mshikamano na kukuza ushirikiano wa kiuchumi,” amesema Ndengo na kuongeza kuwa katika muongo mmoja uliopita, nchi hizo mbili biashara imepanuka kwa kiasi kikubwa.
Amesema Uturuki inatambulika kimataifa kwa uvumbuzi na ubora wake katika uzalishaji wa chuma, wakati Tanzania inakabiliwa na ukuaji wa haraka wa viwanda na upanuzi wa miundombinu.
Amesema ushirikiano huo hautaimarisha tu minyororo ya thamani lakini pia kutengeneza ajira na kuhamisha teknolojia hadi Tanzania.
“Chuma bado ni uti wa mgongo wa maendeleo ya viwanda-kusaidia ujenzi, nishati,usafiri, na viwanda. Mahitaji ya

Tanzania ya bidhaa bora za chuma yanaendelea kuongezeka kulingana na miradi mikubwa inayoendelea.
Makamu Mwenyekiti wa ujumbe huo, Ugur Dalbeler amesema uchumi unaokuwa wan chi hiyo unatoa fursa kubwa za ushirikiano na mauzo kwa wauzaji wa Uturuki.
Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi katika Jangwala Kusini mwa Afrika na kwamba Uturuki inaendelea kuuza bidhaa zenye thamani yad ola milioni 216 kwenda Tanzania na uwezo unaendelea kuongezeka.
Amesema katika sekta ya chuma wanasafirisha tani 40,000 mwaka 2024 na tani 19,400 katika miezi saba ya mwanzo yam waka huu, jumla ya mauzo ya Tanzania ya bidhaa zilizoingizwa inaendelea kufikia dola bilioni 16.6.
Balozi wa Uturuki nchini, Dk Bekir Gezer amesema Uturuki inaahidi kuendeleza biashara na kuwa bora kwa kuwa Tanzania ni eneo bora kwa uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.
