MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: REA Yajivunia Mafaniko ya usambazji wa Teknolojia za Nishati Safi kwa Wananchi Vijijini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > REA Yajivunia Mafaniko ya usambazji wa Teknolojia za Nishati Safi kwa Wananchi Vijijini
Makala

REA Yajivunia Mafaniko ya usambazji wa Teknolojia za Nishati Safi kwa Wananchi Vijijini

Author
By Author
Share
4 Min Read
Issa Sabuni na Lucy Ngowi
Dodoma: KATIKA maonesho ya  Kilimo yajulikanayo kama Nane Nane, kwa mwaka huu 2025 jijini Dodoma,  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umejivunia mafanikio makubwa katika kuhamasisha na kuelimisha wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na usambazaji wa umeme kwenye vitongoji na vijijini.
Akizungumza katika banda la REA, Ofisa Upimaji Mwandamizi, Hussein Shamdas, anasema mwitikio wa wananchi mwaka huu umekuwa mkubwa zaidi, jambo linalodhihirisha jinsi Watanzania wanavyoendelea kuelewa umuhimu wa nishati safi na salama kwa afya na mazingira.
“Sisi REA tumepata mafanikio makubwa sana mwaka huu. Tumepokea wananchi wengi waliokuja kujifunza kuhusu nishati safi, umeme na teknolojia mpya zinazowalenga hasa watu wa vijijini,” anasema.
Habari Picha 9054
Umeme Vijijini: Safari ya Mafanikio
Tangu kuanzishwa kwa REA mwaka 2007, vijiji vilivyokuwa na umeme vilikuwa 234 pekee. Hadi sasa, vijiji 12,318 vimeshapata umeme, huku baadhi ya vitongoji pia vikiwa vimeunganishwa. Juhudi zimehamia katika kufikisha umeme kwa vitongoji vilivyobaki, ambavyo vinakadiriwa kuwa kati ya asilimia 48 hadi 49.
Mapinduzi ya Nishati Safi ya Kupikia
REA imekuja na suluhisho la changamoto sugu kwa wakazi wa vijijini kupitia teknolojia za majiko banifu, majiko ya umeme yanayotumia umeme kidogo (Induction cookers) na pressure cookers za kisasa.
Pia yapo majiko banifu; haya yanatumia mkaa kidogo au kuni chache, lakini yanafanikiwa kutoa nishati kubwa ya kupikia kwa ufanisi na kwa gharama ndogo.
Aidha, teknolojia ya Induction cooker hutumia umeme kidogo sana kwa sababu nishati huingia moja kwa moja kwenye chakula kupitia sumaku tofauti na majiko ya zamani.
Vilevile, pressure cookers za kisasa zinatumika hata kwa kupika ugali, kukaanga nyama na chakula kingine, huku zikitumia umeme mdogo kwa ufanisi mkubwa.
Habari Picha 9048
Nishati kwa Kila Mtanzania
Kuhusu nishati kwa kila mtanzania, Shamdas anasema lengo la REA ni kuhakikisha hakuna Mtanzania anayebaki nyuma.
Katika maonesho haya, wameshirikiana na wadau waliokuja na mitungi midogo ya gesi inayoweza kutumika kwa familia ndogo kwa hadi siku mbili kwa bei ya chini kuanzia TSh 2,500 tu.
“Mtanzania sasa anaweza kuchagua aina ya nishati anayoimudu  hata kama ni kwa matumizi ya siku moja. Sasa nishati safi imefika hadi ngazi ya rejareja,” anasema.
 Mikopo ya Ujenzi wa Vituo vya Mafuta Vijijini
Akizungumzia mikopo ya ujenzi wa vituo vya mafuta vijijini anasema, REA pia imeanzisha mpango wa utoaji mikopo nafuu ya hadi TSh milioni 133 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta vijijini.
Lengo ni kukomesha uuzaji wa mafuta kwa chupa au vidumu  hali inayosababisha ubora duni wa bidhaa na hatari kwa usalama.
Mkopo huo hutolewa kwa wananchi wenye eneo la angalau mita za mraba 924, na unaweza kurejeshwa ndani ya miaka saba, baada ya kipindi cha matarajio cha miezi sita, kwa riba nafuu ya asilimia tano hadi saba.
“Hii ni fursa kwa wakazi wa vijijini, hususan wanawake, kuwa wajasiriamali halisi kupitia ujenzi wa vituo vya mafuta vilivyo salama na vya kisasa,” amesema Shamdas.
Kuendelea Kuboresha
REA inasisitiza kuwa iko tayari kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wananchi na wadau ili kuboresha zaidi teknolojia na huduma zake. Hii ni dhamira ya kuhakikisha kila Mtanzania — mjini au vijijini — anapata fursa ya kutumia nishati safi, salama na rafiki kwa mazingira.

You Might Also Like

Martha Mariki Achukua Fomu Kutetea Nafasi Yake Katavi

Abubakar Assenga Aomba Ridhaa Ya Wananchi Wa Kilombero Wamchague Tena

IITA,TARI, TPHPA Wapambana Kudhibiti Ugonjwa Wa Fungashada Ya Migomba

Wanachuoni Katika Mawasilianao ya Utamaduni kati ya China na Afrika

OSHA yaelimisha sheria mahala pa kazi kwa JOWUTA

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article DKT. Biteko Azindua Mradi Utakaowakwamua Vijana Kiuchumi Katika Maeneo Yanayopitiwa Na Bomba La Mafuta Ghafi  (EACOP)
Next Article Umeme Jua Kuchoche Uchumi Maeneo Ya Vijijini
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Apongeza Jeshi La Magereza Kurasimisha Ujuzi Kwa Wafungwa
Habari August 27, 2025
Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano
Habari August 27, 2025
Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini
Habari August 27, 2025
VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Habari August 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?