MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: SADC Yasisitizwa Kuhusu Safari ya Ukombozi wa Kiuchumi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > SADC Yasisitizwa Kuhusu Safari ya Ukombozi wa Kiuchumi
Habari

SADC Yasisitizwa Kuhusu Safari ya Ukombozi wa Kiuchumi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
1 Min Read
Na Mwandishi Wetu
NCHI wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimetakiwa kudumisha mshikamano na utekelezaji thabiti wa malengo yao ili kufanikisha ukombozi wa kiuchumi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Profesa Amon Murwira, ametoa wito huo jijini Antananarivo, Madagascar, alipokuwa akikabidhi uenyekiti wa Baraza la Mawaziri kwa mwenzake wa Madagascar,  Rasata Rafaravavitafika, Tanzania iliwakilishwa na Balozi Mahmoud Thabit Kombo.
Profesa Murwira alikumbusha kuwa mafanikio ya jumuiya hiyo yanahitaji dhamira ya kweli na kushinda changamoto zilizopo.
Amewakumbusha washiriki kuhusu maono ya waanzilishi wa SADC kama Mwalimu Julius Nyerere na Robert Mugabe, akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kikanda.
Katibu Mtendaji wa SADC, Elias  Magosi, ameeleza kuwa mkutano huo umejikita katika tathmini ya utekelezaji wa dira ya maendeleo, hususan kwenye viwanda, biashara na ushirikiano.
Ametaja changamoto za sasa kama vile mabadiliko ya kisiasa kimataifa, ongezeko la kodi, na kupungua kwa misaada ya wahisani, akihimiza nchi kujitegemea zaidi.
Aidha, ameeleza kuwa SADC inaendelea kuimarisha sekta ya biashara ndogo na za kati, ambazo zinachangia ajira kwa vijana na wanawake, ingawa zinakumbwa na changamoto za ujuzi, mitaji na masoko.
Ili kukabiliana nazo, jumuiya hiyo imeandaa mkakati wa kuongeza ushindani ndani ya soko la Afrika (AfCFTA).

You Might Also Like

Usafirishaji Wa Mizigo SGR Mbioni Kuanza

Ufanisi Wa TANESCO Katika  Utekelezaji Na Usimamizi Wa Miradi Umeleta Mfumo Madhubuti Wa Nishati- Ndejembi

Changamoto uchakataji Mkonge kupatiwa ufumbuzi

Chiku Athumani Aahidi Kusimamia Afya na Elimu kwa Umakini

Lugendo Awataka Wananchi Kujenga Tabia Ya Kufanya Usafi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Dodoma Yazizima Wakati Samia, Nchimbi  Wakichukua Fomu Ya Urais
Next Article VETA kushirikiana na Toyota Tanzania kuboresha mafunzo ya ufundi magari
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?