Na Lucy Lyatuu
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), limesema sekta ya bahari ina fursa nyingi ambazo wananchi wamekuwa hawazifahamu ikiwemo maeneo ambayo wanaweza kusoma na kupata ajira kwa urahisi zaidi na kwamba inaongoza kwa mchango mkubwa kiuchumi hasa katika shughuli za usafirishaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo
Mohamed Salum amesema
hayo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam 2025, maarufu kama ‘Saba Saba’ alipotembelea banda la TASAC
Amesema nchi ina upungufu mkubwa wa wataalamu kupitia sekta hiyo na kwamba zipo ajira na fursa mbalimbali.

Ameongeza kuwa duniani kote kuna upungufu wa mabaharia kwa mujibu wa takwimu za uhitaji mabaharia hawajawahi kutosha kwenye Meli.
Amewataka wananchi kutembelea banda la TASAC kwa lengo kufahamu sekta ya bandari na mchango wake katika uchumi katika nchi.
TASAC ina majukumu mbalimbali ikiwemo majukum Udhibiti wa usafiri majini pamoja na kuchagiza sekta usafiri nchini.
Hivyo aliwaomba wananchi kutembelea katika Banda TASAC lililopo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ili waweze kufahamu sekta ya bandari na mchango wake katika uchumi.
“Tunawakaribisha watu waje kutembelea banda letu ili waweze wafahamu na kujua kuna fursa gani katika sekta ya bahari .
Nchi yetu ya Tanzania inaupungufu mkubwa wa wataalamu kupitia sekta hii zipo ajira na fursa mbalimbali nyingi.

“Duniani kote kuna upungufu wa mabaharia kwa mujibu wa takwimu za uhitaji mabaharia hawajawahi kutosha kwenye Meli”
Aidha amesema
“Jukumu kubwa la TASAC ni Udhibiti shughuli za usafirishaji majini kwa kuusajili vyombo vinavyojengwa nchini na kuvikagua kila hatua na kuvipa vyeti vya ubora”amesema Salum
Pia amesema wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo pamoja na ukaguzi wa meli za kimataifa zinazokuja nchini.