MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Rais Mwinyi Ajionea Mifumo Mbalimbali Banda La Ofisi Ya Waziri Mkuu Sabasaba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Rais Mwinyi Ajionea Mifumo Mbalimbali Banda La Ofisi Ya Waziri Mkuu Sabasaba
Habari

Rais Mwinyi Ajionea Mifumo Mbalimbali Banda La Ofisi Ya Waziri Mkuu Sabasaba

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na  Mwandishi Wetu
 RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu lililopo katika Maonesho ya 49 ya Biashara  maarufu kama sabasaba   yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Katika banda hilo, Dkt. Mwinyi ameona mifumo mbalimbali ikiwemo Mfumo wa Ramani za Vihatarishi vya Maafa Vinavyotokana na Mabadiliko ya Tabia nchi umeandaliwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa masharti ya kifungu cha 31(2)(a) cha Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Sura ya 242 kinachotoa wajibu kwa Wizara, Idara, taasisi za Serikali, Tawala za Mikoa, na mamlaka za Serikali za mitaa kujumuisha katika mipango na bajeti zao hatua za kuzuia na kupunguza madhara ya majanga na kujiandaa kukabiliana na maafa.
Mfumo huo unatoa taarifa za vihatarishi vya maafa kwa kutumia teknolojia ya mifumo ya taarifa za kijiografia zinazowezesha utambuzi wa maeneo yaliyo katika hatari zaidi ya kuathirika na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi kama mafuriko, ukame na ongezeko la joto.
 Kwa kuzingatia viashiria vya kijamii, kiuchumi, kimazingira na kiteknolojia.
 Lengo la mfumo huo ni kusaidia taasisi za serikali, sekta binafsi, mashirika ya maendeleo na wadau wengine kutumia ipasavyo ramani hizo katika upangaji na utekelezaji wa mipango na mikakati katika uendelezaji wa miundombinu, usimamizi wa matumizi ya ardhi na shughuli za kiuchumi.
Aidha, Dkt. Mwinyi ameelezwa kuhusu mfumo wa taarifa ya haraka dhidi ya moto, mfumo unaolenga kushughulikia changamoto ya ucheleweshwaji wa taarifa kuwafikia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutokana sababu mbalimbali ikiwemo kutofahamu namba ya dharura na taharuki pindi tukio la moto linapotokea, vilevile katika maeneo yenye vikwazo vya matumizi ya simu za mkononi kama vile mashuleni na magereza.
Mfumo huo umeunganishwa moja kwa moja na mtungi wa kuzimia moto, ambapo mara mtungi unapochukuliwa kwa ajili ya kudhibiti moto, mfumo hutuma taarifa ya tahadhari kwa njia ya simu na ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) ukionesha eneo la tukio kwa Jeshi la Zimamoto na wadau husika bila kuhitaji uingiliaji wa binadamu.
Vilevile, Rais Mwinyi ameelezwa kuhusu Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Watu Wenye Ulememavu ambapo ni programu ya kielektroniki inayojumuisha Usajili wa Watu wenye ulemavu, Hifadhi salama ya Taarifa za Watu wenye ulemavu pamoja na Kuhamisha Taarifa za Watu wenye Ulemavu.
Aidha, faida za mfumo huo unalenga kupunguza gharama za usafiri na vifaa kwa ajili ya usafiri, kutoa takwimu sahihi zinazosaidia serikali, kupanga na kutekeleza sera kwa ufanisi na kuongeza ujumuishaji wa watu wenye ulemavu kwenye huduma za kijamii na maendeleo.
Rais Mwinyi ametembelea banda hilo kama Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Saba Saba yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam.

You Might Also Like

Mnyororo wa Biashara Kariakoo Unafanywa Na Wageni

Mafunzo Yatolewa Katika Kongamano La Jotoardhi

Ununuzi Wa Ndege Anga Za Kilimo Uanze Sasa-Bashe

VETA Mikumi Yatengeneza Mashine Ya Kuchakata Majani Ya Mifugo

USAID yatoa Dola mil nane Kwa kampuni za Tanzania

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Maabara Ya Mkemia Mkuu Yashauri Wajasiriamali Wa Kemikali
Next Article Tanzania Yafungua Milango Ya Biashara Na Jumuiya Ya Ulaya
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

PSSSF Itaendelea Kuwekeza Kwenye Maeneo Salama Yenye Tija
Habari July 8, 2025
Taasisi Za Umma Zasisitizwa Kuzingatia ubora Wa Mikataba Katika Utekelezaji Wa Majukumu Yao
Habari July 8, 2025
VETA Yang’ara Sabasaba
Habari July 8, 2025
Mashine Kusaidia Uuzaji Vinywaji Bila Muuzaji
Habari July 8, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?