Na Lucy Lyatuu
MAMLAKA ya Dawa Na Vifaa Tiba (TMDA) imesema kwa sasa inasimamia masuala yote yanayohusu bidhaa za tumbaku Ili kuhakikisha wananchi wasiendelee Kupata madhara wanapotumia bidhaa hizo.
Mkurugenzi Mkuu Wa TMDA Dk Adam Fimbo amesema hayo katika Banda la TMDA lililoko viwanja vya maonesho ya 49 ya Biashara Ya Kimaraifa maarufu kama sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam.
Amesema ni jukumu la Mamlaka hiyo inafuatilia usalama Wa dawa kwenye masoko kwa maana dawa yoyote anayotumia mwanadamu haipaswi kuwa na madhara.
” TMDA jukumu lao ni kuhakikisha dawa hiyo inafanya kazi iliyokusudiwa kwa maana ya kutibu lakini sio kuleta madhara kwa binadamu,” amesema.

Amesema hivyo TMDA inafanya kazi kubwa ya kuweza kubaini madhara yoyote yanayoweza kujitokeza kwa watu.
Ameongeza kuwa pia Mamlaka inapima bidhaa za dawa kwenye maabara zilizopo nchini ambapo zimethibitishwa na Shirila La Afya Duniani (WHO) Ili Kufanya kazi ya kupima ubora Wa dawa kwenye Soko na kuruhusu zile tu ambazo zimekidhi viwango vilivyowekwa.
Amesema wako katika maonesho hayo ya sabasaba Ili kuelimisha watanzania kuhusu sekta ya Dawa Ili kulinda afya ya jamii.
“Majukumu Yetu ninkusajili dawa zinazoingia nchini na hakuna dawa inayoweza kuingia bila kusajiliwa na Mamlaka,” amesema na kuongeza kuwa usajili unahusisha Kufanya tathmini ya ubora,usalama na ufanisi ,” amesema.
Aidha amesema Mamlaka hiyo hufanya ukaguzi kwa dawa zilizosajiliwa ikiwa ni kwenye masoko,mipaka ya nchi, maduka ya Dawa,hospitalini na Kila eneo Ili kuhakikisha bidhaa inayofika kwa watanzania ni salama,bora na fanisi.