– Pamoja Na Mfuko Wa Elimu Kwa Taifa
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA), imewaalika wananchi kutembelea banda lake kujifunza jinsi Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) pamoja na Mfuko wa Elimu kwa Taifa unavyofanya kazi kwa ajili ya ujenzi wa taifa na elimu nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano ba Mawasiliano kwa Umma wa mamlaka hiyo, Bestina Magutu ametoa wito huo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam.
Akifafanua hilo amesema mfuko huo wa elimu kwa taifa kazi yake kubwa ni kutafuta rasilimali kwa maana ya fedha na vifaa, baada ya kutafuta zinapelekwa kwenye ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa maana ya nyumba za walimu, matundu ya vyoo, mabwalo, madarasa na vifaa vingine vya elimu.
Amesema kazi ya SDF ni kutoa udhamini wa mafunzo kwa vijana na wanawake wa kitanzania ambayo yamegusa maeneo makuu sita.
Ametaja maeneo hayo kuwa ni ujenzi, uchukuzi, huduma za utalii pamoja na ukarimu, usindikaji wa bidhaa pamoja na kilimo.
“Katika maonesho haya tupo na wadau wawili ambao walipata huu udhamini wa mfuko wa SDF kwenye maeneo ya usindikaji wa chakula kwa maana ya viungo pamoja na kikimo cha uyoga.
” Wapo kwa ajili ya kuonesha namna gani ambayo wamepata mafunzo hayo na yamewanufaisha kwamba wanaweza kujitegemea wao wenyewe,” amesema.