Na Danson Kaijage
DODOMA: SERIKALI imeimarisha upatikanaji wa nishati nchini ikiwemo kukamilisha mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP)

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo wakati akihitimisha shughuli za Bunge Jijini Dodoma Juni 27, mwaka huu 2025.
Samia amesema hayo yote yamefanyika kutokana na umuhimu wa Sekta hiyo kwa maendeleo ya nchi.

Pia amesema serikali imekamilisha upelekaji wa umeme katika Vijiji vyote 12,318 nchini.
Na kwamba, msukumo uliofanywa na serikali katika sekta ya nishati umewezesha uzalishaji wa umeme kuongezeka hadi kufikia megawati 4031.71 kutoka megawati 1,601.84 mwaka 2020.

“Hali hii imechangiwa na miradi mbalimbali ya uzalishaji umeme ukiwemo mradi wa kielelezo wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere wenye megawati 2115,
“Vilevile mradi wa Kinyerezi I Extension wa megawati 185 na mradi wa Rusumo ambao tumeutekeleza kwa ushirikiano wa Nchi tatu za Tanzania, Burundi na Rwanda kwa mgawanyo wa megawati 26.67 kwa kila Nchi,” amesema.

Vile vile maelezo ya Samia ni kwamba, serikali imekamilisha miradi ya usafirishaji umeme ya kutoka Singida hadi Arusha, Geita hadi Nyakanazi, na Julius Nyerere hadi Chalinze.
Miradi mingine ni Nyakanazi hadi Kigoma, Tabora hadi Urambo, Rusumo hadi Nyakanazi na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kwenye njia ya Reli.

Amesema mafanikio hayo yameongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa mijibu wa Rais Samia, serikali imeiunganisha mikoa ya Kigoma na Katavi na gridi ya Taifa.
Amesema kwa sasa Serikali inapeleka umeme kwenye Vitongoji ambapo vitongoji 33,657 tayari vimeshafikishiwa umeme kati ya Vitongoji 64,359 sawa na asilimia 
