MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Matumizi Mabaya Ya Dawa Husababisha Usugu Wa Vimelea Kwa Wanyama – Dkt. Kitimu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Matumizi Mabaya Ya Dawa Husababisha Usugu Wa Vimelea Kwa Wanyama – Dkt. Kitimu
Habari

Matumizi Mabaya Ya Dawa Husababisha Usugu Wa Vimelea Kwa Wanyama – Dkt. Kitimu

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
ARUSHA: WATAALAMU kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA), mkoani Morogoro wametoa elimu kwa wafugaji wa Mkoa wa Arusha kuhusu mbinu bora za kudhibiti homa ya kiwele,
Pia namna ya kukabiliana na changamoto ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.
Mhadhiri kutoka SUA ambaye pia ni mtafiti katika Mradi wa NANO COM,  Dkt. Shedrack Kitimu amesema chanzo kikuu cha Usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA), ni matumizi mabaya ya dawa kwa binadamu na wanyama.
Vile vile  matumizi ya kupita kiasi, kutokumaliza dozi, na matumizi bila ushauri wa kitaalamu ni miongoni mwa sababu zinazochochea usugu huo.
Amesema baadhi ya wafugaji hutumia dawa zisizo na ubora au zilizokwisha muda wake wa matumizi, huku wengine wakitumia dawa kwa ajili ya kukuza wanyama badala ya matibabu.
Pia amesema usafi hafifu, ukosefu wa uchunguzi sahihi wa magonjwa, na ulaji wa mazao ya mifugo bila kuzingatia muda vinachangia tatizo hilo kuongezeka.
“Uchafuzi wa mazingira kwa kutupa mabaki ya dawa kiholela pia huchochea kuenea kwa vimelea sugu,” amesema.
Naye Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Dkt. Charles Msigwa amesema zaidi ya asilimia 60 ya wafugaji katika eneo hilo wanafuga ng’ombe wa maziwa, huku changamoto ya homa ya kiwele imekuwa tatizo sugu.
Amesema mafunzo hayo yamewasaidia wafugaji kuelewa umuhimu wa kutunza kumbukumbu za matibabu na matumizi sahihi ya dawa.
Kwa upande wake,  Mkazi wa Arusha Martina Mushi, amesema baadhi ya wafugaji hukatisha matibabu ya mifugo ili waendelee na biashara ya maziwa au hutumia dawa zisizofaa, jambo linalochangia usugu wa vimelea.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sivat Agribusiness Ltd. Lopeny Tajiri amesema mafunzo hayo yamewasaidia kutambua dalili za UVIDA na namna ya kuwashauri wafugaji katika kudhibiti homa ya kiwele.
Amesema kampuni yao imepata maarifa yatakayowasaidia kuboresha huduma wanazotoa.
Mradi wa NANO COM unatekelezwa na SUA kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali katika mikoa ya Arusha, Tanga, Iringa, Mbeya na Njombe.
Mradi huo unalenga kuboresha afya ya mifugo, usalama wa maziwa, na kuimarisha uelewa kuhusu UVIDA kwa kutafuta tiba mbadala na kusambaza elimu kwa wadau wa sekta ya mifugo.
UVIDA umeendelea kuwa changamoto kwa afya ya mifugo na usalama wa maziwa nchini, hali inayohitaji hatua za pamoja kutoka kwa wadau wa sekta ya mifugo na afya.
Wafugaji 50 walishiriki kwenye mafunzo hayo, wanawake wakiwa 18 Sawa na asilimia 32.

You Might Also Like

Jeshi La Uhifadhi Wasisitizwa Kuzingatia Misingi ya Haki za Binadamu

TAKUKURU, Manispaa Ubungo Yawafikia Waendesha Bajaji, Bodaboda

Ridhiwani Aiagiza CMA Kushughulikia Migogoro Kwa Haraka, Ufanisi

OUT Yasaini Mkataba Ujenzi Wa Maabara Tatu Za Sayansi

Ridhiwani: Maandalizi Mei Mosi  Yafikia Asilimia 88

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Mgeni Rasmi Mkutano Wa THRAPA
Next Article Daraja La Magufuli Laimarisha Uhusiano Wa Jumuiya Ya China,Tanzania Yenye Mustakabali Wa Pamoja
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Bodi Ya Wadhamini Ya NSSF Yaridhishwa Na Uwekezaji Wa Ubia Na Jeshi La Magereza
Habari May 14, 2025
TPHPA Yaelezea Vipaumbele Vyake
Habari May 14, 2025
TPHPA Tuna Mchango Mkubwa Katika Utoshelevu Wa Chakula – Ndunguru
Habari May 14, 2025
Profesa Ndunguru: Tumewezesha Usafirishaji wa Mazao Mbalimbali Yenye Thamani ya Trilioni 15.6
Habari May 14, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?