Na Waandishi Wetu
Kutokana na mabadiliko ya kibiashara duniani yaliyosababishwa na sera mpya za ushuru za Marekani, Kenya na Tanzania zimeimarisha ushirikiano wao na China, zikiilenga katika soko lake kama fursa muhimu ya kukabiliana na changamoto na kutafuta maendeleo kupitia uchumi na biashara.
Hivyo Wasafirishaji, wauzaji bidhaa nchi za nje kutoka Kenya, wameelekeza macho yao kwenye soko la China.
Ofisa Mkuu Mtendaji wa Idara ya Uhamasishaji wa Uuzaji Bidhaa Nje ya Nchi na Uenezaji wa Chapa ya Kenya (KEPROBA), Floice Mukabana anasema China ni soko kubwa, lengo la Kenya ni kuhakikisha bidhaa zake zinapatikana kote nchini China.
Anasema Kenya imepanga kujikita zaidi katika soko la China kupitia Maonyesho ya Nne ya Kiuchumi na Biashara kati ya China na Afrika (China-Africa Economic and Trade Expo).
Kampuni mbalimbali za Kenya pia ziko mbioni kuchukua hatua mbalimbali, huku Mkurugenzi Mkuu wa Biashara na Uuzaji wa Nje kutoka Kampuni ya Jotim Coffee Limited, Josphine Ndikwe anasema soko la China ni kubwa na lina ushuru unaofaa.
Tangu waanze kuuza kahawa nchini China mwaka 2022, uwezo wao wa kuuza nje umeongezeka kwa kiwango kikubwa, na wamepanga kuingia katika sekta ya uuzaji wa nje wa kahawa iliyochomwa katika siku zijazo.
Mbali na kahawa, maparachichi na chai pia ni bidhaa muhimu ambazo Kenya imepanga kuzisafirisha na kuziuza nchini China.
Tanzania pia imepanga kwa dhati kuimarisha ushirikiano na China katika nyanja mbalimbali.
Katika suala la miundombinu ya usafiri, ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Treni za Mwendokasi (SGR), Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa inayounganisha Dar es Salaam na nchi jirani utaongezwa kasi kwa msaada wa kifedha na kiufundi kutoka China.
Hivyo kusaidia kukuza ushirikiano wa kikanda wa Afrika Mashariki.
Eneo la uchimbaji madini, kampuni za China zinatarajiwa kupanua uwekezaji wao katika uchimbaji wa madini adimu na lithiamu nchini Tanzania.
Katika ushirikiano wa kiuchumi wa bahari, miradi kama vile hifadhi za usindikaji Samaki na upanuzi wa bandari itaanza hatua kwa hatua.
Pia sekta ya nishati mpya, China itasaidia Tanzania kuendeleza miradi ya nishati ya jua na upepo ili kufikia lengo la asilimia 25 ya nishati safi ifikapo mwaka 2030.
Vile vile kwenye uchumi wa kidijitali na ujenzi wa miji mahiri, kampuni kama vile Huawei na ZTE zitaimarisha ushirikiano wao wa mawasiliano na Tanzania.
Pia kwenye sekta ya kilimo, Kituo cha Mfano cha Teknolojia za Kilimo kilichojengwa chini ya msaada wa China kitaongezewa wigo wake, na pande hizo mbili zitafanya utafiti wa pamoja kuhusu kukabiliana na ukame katika kilimo.
Mwonekano wa Daraja la J.P. Magufuli lililoko mkoani Mwanza nchini Tanzania ambalo limejengwa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ikishirikiana na Kampuni ya China Railway 15th Bureau Group Corporation Limited (CR15). Na lilifanikiwa kuunganishwa Oktoba sita,mwaka jan 2024.
Sera mpya za ushuru za Marekani zimeleta athari kubwa kwa uchumi ulimwenguni. Katika hali hiyo, mataifa ya Kiafrika kama Kenya na Tanzania yamepata njia mpya za soko kwa bidhaa zao na kupata msaada wa maendeleo katika nyanja mbalimbali kupitia kuimarisha ushirikiano na China.
Mtindo huo wa ushirikiano umeongeza nguvu kubwa katika kujenga jumuiya ya ngazi ya juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
Hivyo Kupitia kuongezeka kwa biashara, uboreshaji wa miundombinu, na ushirikiano wa viwanda unaolingana, misingi ya ushirikiano kati ya China na Afrika imeimarika kwa kina zaidi.
Na kwamba juhudi hizo zimehimiza kusaidiana na kunufaishana kwa pande zote huku zikisukuma pande zote mbili kwenye njia ya maendeleo ya pamoja,
Zimethibitisha umuhimu wa kujenga jumuiya ya ngazi ya juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
Mwandishi 1: Ning Yi, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).
Barua pepe:02706@shisu.edu.cn
Mwandishi 2: Zhou Li, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Tianjin (TFSU)
Barua pepe: sylvanzhou@foxmail.com