MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: BAKITA Lapongeza Sheria Za Tanzania Kuandikwa Kwa Lugha Ya Kiswahili
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > BAKITA Lapongeza Sheria Za Tanzania Kuandikwa Kwa Lugha Ya Kiswahili
Habari

BAKITA Lapongeza Sheria Za Tanzania Kuandikwa Kwa Lugha Ya Kiswahili

Author
By Author
Share
4 Min Read

Na Mwandishi Wetu

MWANZA: BARAZA la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limepongeza jitihada zinazofanywa na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuhakikisha sheria zote za Tanzania zinaandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Mhariri Mkuu wa Baraza la Kiswahili la Taifa Richard Ntambi, ametoa pongezi hizo alipozungumza na Waandishi wa Habari.

amesema watanzania wengi wanaelewana vizuri kwa kutumia lugha ya Kiswahili hivyo kuwa na sheria zilizo kwenye lugha yao kutasaidia jamii kuzijua sheria hizo na kuzifuata tofauti na sasa ambapo zipo kwenye lugha ya kiingereza ambayo wengi wao hawaifahamu.

“Changamoto kubwa iliyopo hasa katika masuala ya haki na mahakama ni matumizi ya lugha ya kiingereza hasa kwa jamii kutoelewa vyema majadiliano yanayofanyika kwenye mahakama hizo na kwenye hukumu zinazotolewa hali inayosababisha malalamiko mengi.

“Na wengine kulazimika kutumia gharama kupeleka hukumu zao kwa watu kuwasaidia kutafsiri sheria na hukumu zao hivyo haya yote yatamalizika kupitia kazi hii ya matumzi ya Kiswahili mahakamani,”amesema.

Amesema wanatambua changamoto ya uwepo wa misamiati michache ya Kiswahili kukidhi ile ya kiingereza lakini jitihada zinafanyika kuhakikisha misamiati ya Kiingereza inapata misamiati sahihi kwa lugha ya Kiswahili kwa kutafuta kutoka kwenye misamiati ya makabila mbalimbali nchini,

Pale inapokwama wanatumia njia ya utohozi wa misamiati hiyo ya kiingereza kwakuwa ni njia pia inayokubalika.

Kwa upande wake Mwandishi maarufu wa riwaya na kazi za sanaa, Profesa wa Sheria Abdalah Safari amesema kazi hiyo kubwa na nzuri inayofanywa na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria imekuwa ni kilio cha muda mrefu cha Watanzania wengi na wadau wa Sheria na Haki.

Profesa Safari ambaye pia ni Wakili, amesema baada ya kazi hiyo sasa ni muhimu kuwa na kamusi ya sheria kwa Kiswahili ingawa tayari Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria imetengeneza Istilahi za Kiswahili ambazo zinatakiwa pia kupitiwa kwa pamoja na wataalamu wa  sheria na lugha ili kujiridhisha na usahihi wake .

“Pamoja na kutengenezwa kwa istilahi hizo za kiingereza kwa lugha ya Kiswahili sasa ni wakati wa kufikiria kitu kikubwa zaidi kama kamusi rasmi ya sheria kwa kiswahili ili kuwezesha hata kazi ya ufasiri kuwa nyepesi na kujenga uelewa wa pamoja kwa kila mtu na kila mdau wa sheria,” amesema.

Amesema Waingereza walitawaliwa na Warumi na kulazimishwa kutumia lugha ya kilatini kwenye sheria zao lakini baada ya kujikomboa wakagundua mtu anafanya vizuri jambo kwa lugha mama hivyo wakabadilisha, kwahiyo na Watanzania lugha mama ni Kiswahili.

“Sheria inasema kutojua sheria sio utetezi lakini kama mimi siijui sheria na nikavunja maana yake siunanionea? Hivyo kuwa na sheria za Kiswahili kutaleta haki kwa watu wote maana watakuwa wanaweza kuzisoma sheria na kuzielewa na kuzifuata,” amesema.

Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria inaendelea kutekeleza maazimio ya Serikali iliyoyatoa Mwaka 2021 kupitia Bunge laTanzania baada ya kupitisha marekebisho ya Sheria ya Tafsiri za Sheria ambapo pamoja na mambo mengine iliweka sharti kwamba lugha ya sheria sasa ni Kiswahili.

 

 

 

You Might Also Like

Bajeti ya TUGHE 2025 Yaidhinishwa

SOKO LA MADINI LA 43 LA ZINDULIWA TUNDURU RUVUMA.

Shule 216 Za Serikali Zatumia Nishati Safi Ya Kupikia – Kapinga

Tume Ya Kurekebisha Sheria Tanzania Kuipitia Sheria Ya Takwimu

Watanzania wasisitizwa kulinda mazingira ya miundombinu ya umeme

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kikosi Kazi Maalumu Cha Kupitia Muongozo Wa Ufasili Wa Sheria Chazinduliwa
Next Article Ofisi Ya Mwandishi Mkuu Wa Sheria Yakamilisha Rasimu Ya Sheria 446 Kwa Lugha Ya Kiswahili
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?