Na Danson Kaijage.
DODOMA: MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la ViwangobTanzania ( TBS), Dkt. Ashura Katunzi amesema watumiaji wa vilevi huvitumia kiholela huku wakinywa kupita kiasi jambo linalofanya vionekane havina ubora.
Dkt. Katunzi amesema hayo alipokuwa akitoa taarifa za mafanikio kwa miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Idara ya Habari -MAELEZO.
Amesema imebainika kuwa vinywaji vingi vikali havipo chini ya kiwango isipokuwa vichache vimekutwa vina kiwango cha chini cha kilevi tofauti na inavyotakiwa.

“Tumefanya ukaguzi katika maduka mengi ya vinywaji vikali imebainika kuwa vinywaji hivyo vingi vina ubora ila vichache havina ubora kutokana na kukutwa kiwango chake cha kilevi kipo chini tofauti na inavyotakiwa hivyo hapo inaonesha kuwa mlaji anakuwa amepunjwa kilevi,” amesema.
Amesema katika kipindi cha miezi sita iliyopita TBS imeteketeza bidhaa ambazo zipo chini ya kiwango zenye thamani ya kiasi cha Sh.Bilioni 1.5.
Amesisitiza kuwa Shirika hilo limekuwa likifanya kazi kubwa ya kuhakikisha viwango vya ubora wa bidhaa zinazotumiwa ni bora kwa walaji wa bidhaa hizo.


Katika hatua nyingine amesema kuwa Shirika hilo limekuwa likitenga kiasi cha Sh. Bilioni 350 kila mwaka kwa ajili ya kuwawezesha wajasiliamali wadogo