Na Mwandishi Wetu
PWANI: WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Chalinze ameshiriki Maulid ya Kumswali Mtume Muhammad yaliyofanyika Mkuranga, Pwani.
Ridhiwani amesema maulid hayo yameandaliwa chini ya Waziri wa Ujenzi, Abdalah Ulega na Uongozi wa Baraza Kuu la Waislam wa Tanzania ( BAKWATA, Wilaya ya Mkuranga, paamoja na viongozi mbalimbali.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa ya kuhudhuria na kupata nafasi ya kushiriki kaswida na Madrasa yangu ya Qadiriyah Ya Bagamoyo kwa Sheikh Ramiyah,” amesema Ridhiwani.

