MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Trilioni 1.2 kuboresha miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Trilioni 1.2 kuboresha miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam
Uncategorized

Trilioni 1.2 kuboresha miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
3 Min Read

Na Mwandishi wetu,DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameeleza kwamba takribani shilingi trilioni 1.2 zitatumika kwaajili ya kuboresha miundombinu kupitia mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es salaam Awamu ya Pili (DMDP Phase II) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mkopo wa masharti nafuu.

Mchengerwa ameyasema hayo katika viwanja vya Mwembeyanga alipokuwa akishuhudia hafla ya utiaji Saini wa mikataba ya ujenzi wa barabara katika Halmashauri 5 za Mkoa wa Dar es salaam ambapo zaidi ya Km. 250 za kiwango cha lami zitajengwa, Km. 90 za mifereji ya maji, vituo vya mabasi 9, masoko 18, ujenzi wa madampo 3 ya kisasa kwaajili ya kuboresha usimamizi wa taka ngumu yatajengwa.

“Mradi huu unatekelezwa kwa gharama za shilingi trilioni 1.1822 ambapo trilioni 1.03 ni mkopo kutoka benki ya Dunia na shilingi bilioni 143 ni ruzuku kutoka Serikali ya Uholanzi, pia malengo ya Serikali kupitia mradi wa DMDP awamu ya pili ni kuboresha miundombinu ya msingi katika Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es salaam pamoja na kuzijengea uwezo wa utoaji huduma kwa wananchi kupitia utekekezaji wa miradi hii”, amesema Mchengerwa.

Aidha, Waziri amewataka TARURA kusimamia utekelezaji wa miradi kwa ufanisi pamoja na kuwasimamia Makandarasi kama ilivyofanyika katika utekelezaji wa miradi ya DMDP awamu ya kwanza ambapo imepelekea wabia wa maendeleo (Benki ya Dunia) kutuamiini na kutupatia fedha za utekelezaji wa DMDP awamu ya pili katika Halmashauri zote tano.

Pia,Mchengerwa amewataka wataalam kuhakikisha miradi inazingatia mahitaji ya wananchi ili kuepuka miradi inayojengwa na kukamilika inaachwa bila kutumika kwa sababu ya kukosa ushirikishwaji wa wananchi, amewakumbusha kuwa miradi ya DMDP izingatie thamani ya mradi.

Akitoa salamu zake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, Jafari Wambura Chege amesema Kamati itaendelea kutoa ushirikiano kwa Waziri ili waweze kuendelea kutatua kero za wananchi zinazowakabili katika maeneo yao kupitia Afya, Elimu na Miundombinu.

“Waziri Kamati inatambua mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uboreshaji wa sekta ya miundombinu na katika kudhihirisha hilo leo tunashuhudia utiaji Saini wa miradi ya DMDP awamu ya pili katika Halmashauri zote tano za Mkoa wa Dar es salaam”.Amesema, Chege.

Awali alipokuwa akitoa taarifa yake

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa TARURA na Mratibu wa Miradi ya Benki ya Dunia Mhandisi Humphrey Kanyenye amesema katika utekelezaji wa mradi awamu ya kwanza Halmashauri za Manispaa ya Temeke, Kinondoni na Ilala zilinufaika ambapo takribani Km. 207 za barabara zilijengwa kwa kiwango cha lami, Km 75.2 mifereji ya maji ya mvua iliboreshwa, kituo cha afya, masoko 10 ya kisasa, maeneo 6 ya wazi pamoja na viwanja viwili vya mchezo vilijengwa.

You Might Also Like

Kapinga : Bei ya umeme Tanzania ni nafuu kuliko nchi nyingine Afrika Mashariki

Prof.Mwakalila azungumza na wanafunzi wapya wa MNMA asisitiza uadilifu na uzalendo

Hakuna Vituo Bandia vya Kuandikisha Wapigakura:Mchengerwa

Jaffo :Wafanyabiashara Tanzania, Iran watakiwa kushirikiana kwa pamoja katika Biashara, Uwekezaji

Waziri Jenista akabidhiwa ofisi rasmi na Ummy Mwalimu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Samia Kalamu Award yasogeza Mbele
Next Article TARI Yanufaisha Wadau Wa Kilimo, Ugunduzi Wa Mbegu Bora Na Za Kisas
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Uongozi CHADEMA Kanda Ya Kati Upo Imara
Habari May 18, 2025
Msisubiri Kupewa Amri, Ufanyaji Usafi Kwenye Maeneo Yenu – Lugendo
Habari May 18, 2025
Akili Bandia Yachochea Ushirikiano Kati Ya China, Afrika
Makala May 18, 2025
Madaktari Toka China Waleta Matumaini Barani Afrika
Makala May 16, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?