MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt Yonaz Awakumbusha Vijana Kulinda Afya Zao Katika Mapambano Dhidi Ya Ukimwi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt Yonaz Awakumbusha Vijana Kulinda Afya Zao Katika Mapambano Dhidi Ya Ukimwi
Habari

Dkt Yonaz Awakumbusha Vijana Kulinda Afya Zao Katika Mapambano Dhidi Ya Ukimwi

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu , Kazuramimba Kigoma
KATIBU Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi, amewaasa vijana kulinda afya zao na kuepuka tabia hatarishi ili kupunguza maambukizi mapya ya VVU, kwa kuzingatia kuwa ni kundi linaloongoza kuwa hatarini zaidi nchini Tanzania.
Dkt. Yonazi ameyasema hayo  wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Afua za UKIMWI Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma alipoambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Dkt. Adam Mrisho, timu ya wataalam kutoka Ofisi yake, Wizara ya Afya, TAMISEMI na Ofisi ya Mkoa huo.
Habari Picha 13372
Aidha amepata wasaa kutembelea Kituo cha Maarifa Kata ya Kazuramimba mkoani humo kinachotoa huduma za masuala ya VVU na UKIMWI, na kukutana na vijana wanaotekeleza afua za UKIMWI kupitia vikundi vya uzalishaji mali kwa lengo la kujiinua kiuchumi na kujiletea maendeleo yao.
Akiwa katika kituo hicho, Dkt. Yonazi amepokea taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kikundi, Billy Sekibaha, kuhusu shughuli zinazofanywa na kikundi hicho ikiwemo za biashara ndogondogo za kuuza dagaa pamoja na shunguli za ushonaji wa nguo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kuondokana na dhana ya utegemezi.
Amesisitiza kuwa, kundi la vijana linategemewa na Taifa katika shughuli za uzalishaji mali na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla hivyo ni vyema vijana wakaendelea kujilinda na kulinda wengine kwa kutambua hali zao na endapo wakagundulika kuwa na maambukizi ya VVU inashauriwa kuanza kutumia dawa mapema.
Habari Picha 13373
“Mnafanya kazi nzuri sana, endeleeni kuchangamkia uwepo wa mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zenu ili kuwafikia wateja wengi zaidi na kujitangaza kitaifa na kimataifa,” alisisitiza Dkt. Yonazi
Kwa upande wake Mtendaji  wa TACAIDS, Dkt. Adam Mrisho amewapongeza vijana hao kwa kazi nzuri wanazofanya na kusisitiza kuwa Tume itaendelea kuwawezesha vijana kiuchumi na kuwajengea uwezo ili kuendeleza mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU na kufikia lengo la kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.
Habari Picha 13374
Habari Picha 13375
Habari Picha 13376
Habari Picha 13377

You Might Also Like

Majiko Banifu 1000 Kuuzwa Kwa Bei Ya Ruzuku Katika Maonesho Ya Madini Geita

Naibu Waziri Katambi Asisitiza Ufanisi na Ubunifu Kwenye SIDO

Midea Group Yafungua Duka Mlimani City Dar Es Salaam

TRA Kupambana Na Wakwepa Kodi Kupitia Bandari Bubu

Mbegu Bora za Miwa Zenye Tija ya Tani 200 kwa Hekta Zaendelea Kuwanufaisha Wakulima

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Maji Yageuka Gesi, Lusano Aibua Ubunifu wa Nishati Safi
Next Article Bunifu ya dawa ya mayai yapunguza hasara kwa wafugaji wa kuku
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Bunifu ya dawa ya mayai yapunguza hasara kwa wafugaji wa kuku
Makala August 22, 2026
Maji Yageuka Gesi, Lusano Aibua Ubunifu wa Nishati Safi
Makala August 22, 2026
Bunifu Ya Dawa Ya Mayai Kupunguza Hasara Kwa Wafugaji Wa Kuku
Makala August 22, 2026
TTCL Yazindua Awamu Ya Pili,’Faiba Mlangoni Kwako’ Yasisitiza Kupanua Wigo Wa Huduma
Habari August 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?