MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TAWIA na MAIPAC washirikiana kuadhimisha Siku ya Wajane, wapanga kupanda Mlima Kilimanjaro
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TAWIA na MAIPAC washirikiana kuadhimisha Siku ya Wajane, wapanga kupanda Mlima Kilimanjaro
Habari

TAWIA na MAIPAC washirikiana kuadhimisha Siku ya Wajane, wapanga kupanda Mlima Kilimanjaro

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Mwandishi wetu, Arusha
TAASISI ya Wajane Tanzania (TAWIA) imeanza rasmi maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wajane Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Juni 23, mwaka huu 2026 mkoani Kilimanjaro, huku ikiingia ubia na Taasisi ya Wanahabari ya usaidizi wa jamii za pembezoni (MAIPAC) ili kuhakikisha tukio hilo linafanikiwa.
Akizungumza Aprili 3, 2026 katika ofisi za MAIPAC jijini Arusha, Mkurugenzi wa TAWIA, Rose Sarwatt, amesema maandalizi muhimu tayari yameanza, yakilenga kuwakutanisha zaidi ya wajane 500 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Sarwatt amesema Siku ya Wajane Duniani inatambuliwa na Umoja wa Mataifa, na nchini Tanzania imekuwa ikiadhimishwa kwa ushirikiano kati ya TAWIA na Serikali.
Habari Picha 11672
Amebainisha kuwa maadhimisho ya kitaifa mwaka huu yatafanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro, huku ya kimataifa yakifanyika nchini Uingereza.
“Nimekuja MAIPAC kama mmoja wa washirika muhimu wanaofanya kazi na wanawake wajane, hasa kutoka jamii za pembezoni. Ushirikiano huu ni muhimu katika kufanikisha maadhimisho haya,” amesema Sarwatt.
Ameongeza kuwa TAWIA tayari inashirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, lakini bado kuna umuhimu wa kushirikisha mashirika ya kiraia (CSOs) ili kuongeza nguvu ya utekelezaji.
Katika maadhimisho ya mwaka huu, Sarwatt amesema mbali na kufanyika kwa kongamano maalum, wajane watapanda Mlima Kilimanjaro kama ishara ya ujasiri na mshikamano, huku wengine wakipata fursa ya kutembelea hifadhi za taifa.
Aidha, amewataka wadau na wafadhili kujitokeza kusaidia kufanikisha tukio hilo, akieleza kuwa ni la kihistoria na lenye lengo la kuhamasisha haki na ustawi wa wajane nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MAIPAC, Mussa Siwayombe, amesema taasisi hiyo iko tayari kushirikiana na TAWIA, akibainisha kuwa tayari imekuwa ikitekeleza miradi inayowahusisha wajane katika wilaya za Monduli, Longido na Karatu.
“Tutahakikisha tunashirikisha vyombo vya habari kwa wingi ili kuongeza uelewa wa jamii kuhusu Siku ya Wajane na masuala yanayowahusu,” amesema.
Naye Ofisa Utawala wa MAIPAC, Andrea Ngobole, amesema kupitia mtandao wa wanahabari zaidi ya 100, taasisi hiyo itatumia maadhimisho hayo kuhamasisha haki za wajane na umuhimu wa kuandika wosia ili kupunguza migogoro ya kifamilia baada ya vifo.

You Might Also Like

‘Jichunge’ Programu Ya Simu Yenye Mafanikio Katika Kuboresha Matumizi Ya Dawa Kinga Dhidi Ya VVU

Majaliwa Ataka Wafanyakazi Waandaliwe Kwa Mabadiliko Ya Teknolojia

Manyara Kusambaza Mitungi 16,275 ya Gesi kwa Bei ya Ruzuku

Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar

Mpango wa Shule Salama Unaongeza ulinzi Kwa Watoto

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article EAC Yaweka Mguu Chini Ushirikishwaji Wa Wanawake Katika Amani, Ulinzi Na Usalama
Next Article Askofu Chilongani Aitaka Jamii Kutumia Ijumaa Kuu Kusameheana na Kujenga Umoja
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TPHPA Yatumia Mbinu za Kibaiolojia Kudhibiti Gugu Ziwa Victoria
Habari May 24, 2026
Wizara Ya Viwanda Kutekeleza Vipaumbele Saba, Ipo  Miradi Ya Viwanda Ya  Kimkakati
Habari May 22, 2026
Biashara 15 Hazitakiwi Kufanywa Na Wageni Ndani Ya Nchi
Habari May 22, 2026
Wadau wataka mifumo jumuishi kupunguza mzigo wa malezi kwa wenye ulemavu
Habari May 21, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?