MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: DIB: Wenye Amana Benki Zilizofungwa Kulipwa Ndani ya Mwezi Mmoja
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > DIB: Wenye Amana Benki Zilizofungwa Kulipwa Ndani ya Mwezi Mmoja
Habari

DIB: Wenye Amana Benki Zilizofungwa Kulipwa Ndani ya Mwezi Mmoja

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
BODI ya Bima ya Amana (DIB) imesema wananchi waliokuwa na amana katika benki zitakazofungwa au kufutiwa leseni na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hulipwa fidia ya amana zao zilizo katika kiwango cha kinga ndani ya mwezi mmoja baada ya kutangazwa rasmi kufutwa kwa leseni ya benki husika.
Akizungumza kuhusu hilo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma na Mawasiliano wa DIB, Lwaga Mwambande, alisema kiwango cha juu cha amana kinachokingwa na bodi hiyo ni Sh milioni 7.5 kwa kila mteja.
Alifafanua kuwa mteja yeyote mwenye amana isiyozidi kiwango hicho hulipwa fedha zake zote endapo benki yake itafungwa au kufutiwa leseni.
Hata hivyo, alisema kwa wateja wenye amana zinazozidi Sh milioni 7.5, DIB huendesha zoezi la ufilisi ili kudhibiti na kuuza mali za benki husika kwa lengo la kurejesha sehemu ya amana zao.
Mwambande alitoa mfano wa Benki ya FBME iliyofutiwa leseni mwaka 2017, akisema katika awamu mbili zilizopita walilipwa jumla ya asilimia 55 ya madai yao, na novemba 2025 yametangazwa malipo mengine ya asilimia 30, na hivyo kufanya wawe wamelipwa jumla ya asilimia 85 ya madai yao.
Aliongeza kuwa DIB inaendelea kukusanya na kusimamia mali za benki zilizofungwa ili kuhakikisha wateja wanarejeshewa kiwango kikubwa zaidi cha fedha zao kadri inavyowezekana.
Aidha, alisema kuwa kuanzia mwaka jana, bodi hiyo imeanza kutekeleza jukumu la kupunguza hasara mapema kwa kuingilia kati kabla benki haijafikia hatua ya kufilisika au kufutiwa leseni.
Kupitia ushirikiano na Benki Kuu ya Tanzania, DIB inaweza kuidhinisha mikopo au kusaidia kuikopesha benki yenye changamoto ili kurejesha uimara wake wa kifedha na kuiwezesha kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

You Might Also Like

Jeshi la polisi kumhoji anayesambaza taarifa za uongo

Chanzo Cha Bunge Kuridhia Hoja Ya Wanaojifungua Njiti, Kilianzia Hapa

Wanafunzi UDSM, MUM Kushiriki Fainali Ya Kimataifa Mashindano Ya Chinese Brigde

Mwalim: Niko Tayari Kushirikiana na Majaliwa Nikipewa Ridhaa ya Urais

VETA Yawawezesha Vijana Wenye Mahitaji Maalum Kung’ara Katika Fani za Ufundi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TADB Yatoa Elimu ya Kifedha kwa Wananchi na Wanafunzi Tanga
Next Article Mkurugenzi Mkuu Wa NSSF Aongoza Utoaji Wa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii Soko La Tegeta Nyuki
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?