– Amalizie Pale Alipoishia
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Jimbo la Kilombero mkoani Morogoro Abubakar Asenga(CCM)amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena kutetea kiti hicho akiahidi kushughulika na kero za wananchi kwa kiango kikubwa.
Akizungumza mjini Dodoma Juni 27, mwaka huu 2025, amesema ana dhamira ya dhati kushughulika na mambo mbalimbali katika Jimbo la Kilombero.

“Tunaomba dhamana mwaka 2026 mkituchagua tukianza kazi Januari tutapita katika vijini 48 na mitaa 33 kujaribu kuchukua mambo mawili matatu ambayo tutayasukuma.
“Tunawaambia wananchi kwamba sisi sio malaika hatuwezi kufanya kila kitu kwa siku moja lakini tuna uhakika kwamba tunaweza kusukuma baadhi ya mambo muhimu kwa maendeleo ya wananchi wetu,” anaeleza mbunge huyo.
Anaeleza mambo yaliyoshughulikiwa akisema katika jimbo hilo mbunge yoyote alikuwa akiadhibiwa kukaa kwa miaka mitano kisha kutochaguliwa tena kutokana na changamoto ya barabara.
Jambo jingine ni kuhusu wakulima wa miwa akisema tayari wamejengewa kiwanda kipya cha sukari hivyo kuwaondolea adha waliyokuwa wakiipata.
“Serikali ya awamu ya sita chini ya rais Samia Suluhu Hassan ilitoa zaidi ya bilioni 700 ambazo zimefanikisha ujenzi wa kiwanda kipya cha sukari kipo na kinaendelea na rais ameweka jiwe la msingi.
“Asilimia 60 ya wananchi wa Jimbo hilo ni wakulima wa miwa hivyo miwa mingi ilikuwa ikibaki shambani, viwandani kwa sababu kiwanda kilikuwa hakina uwezo wa kuchukua miwa yote ya wakulima shambani
“Bababara zinazotenganisha na wilaya nyingine mojawpao ni barabara ya Mlimba( ya kilometa 112) ya Ifakara hadi Mlimba ambayo imeshapata mkandarasi na nyingine ya Ulanga na Malinyi inayoanzia Kikwawila kupitia Mbasa, Lipangala, Lupiro hadi Malinyi ambayo tayari fedha na wakandarasi wameshapatikana.” anasema.
Jingine ni kujenga Sekondari kila Kata akisema wameshajenga Sekondari 12 katika Kata ambazo hazikuwa na sekondari na zimeshaanza kufanya kazi pia madarasa zaidi ya 150 na shule za msingi nane ambazo ni mpya pia wamejenga shule moja ya ufundi(shule za amali) katika Kata ya Kisawasawa ambayo imekamilika.
Pia wamepeleka umeme katika vijiji vyote na kujenga mradi mkubwa wa umeme unaogharimu kiasi cha Shs. Bilioni 225 ambao utazuia kukatika kwa umeme na rais Samia alishautembelea pamoja na Naibu waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati. Dk. Dotto Biteko.
“Umeme ulikuwa ukikatika siku za nyuma lakini hivi sasa tatizo hilo halipo, tulikuwa pia na shida kubwa katika afya na sasa tumejenga Zahanati 12 vimekamilika na tumepata vifaa na madakari,” anasema Asenga.