Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: WANANCHI wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma kutokana na upungufu wa majengo yanayokidhi kutoa huduma za kimahakama.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Salma Maghimbi amesema hayo alipokuwa akielezea changamoto katika mfumo wa utoaji wa haki ambazo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi..
“Mfano halisi ni Mahakama za Mwanzo Buguruni, Ilala na Ukonga. Bado Tuna upungufu mkubwa majengo ikilinganishwa na mahitaji halisi.Muendelezo wa naboresho unaendelea kwa kujenga majengo mapya,” amesema.
Aidha baadhi ya majengo katika mahakama za mwanzo baadhi ya majengo yake ni duni.
Amesema kwamba pamoja na changamoto hizo, muendelezo wa maboresho na kujenga majengo mapya unaendelea.
,