Na Waandishi Wetu
BARAZA la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) la mwaka 2024 limedhihirisha kuwa Afrika na China ni Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja katika hali zote katika zama mpya.
Hilo linadhihirika kwa kuwa, Nchini China wanazuoni wanazidi kutambua umuhimu wa kuwajulisha watu wa China habari zinazohusu Bara la Afrika.
Hii inatokana na historia yake ndefu na utamaduni wake tajiri. Afrika inastahili kufanyiwa utafiti zaidi.
Pili katika ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya hali zote katika zama mpya baina ya China na Afrika, kuwasiliana na kufundishana kwa utamaduni ni sehemu isiyokosekana, pia msingi wa urafiki kati ya watu wa China na Afrika.
Siku zote wanazuoni wa pande mbili wanabeba jukumu muhimu la kueneza ujuzi na kusukuma mbele mawasiliano ya utamaduni.
Hivyo mawasiliano kati ya China na Afrika yalianza muda mrefu, Lakini utafiti unaohusu Afrika nchini China haukuanza mapema ukilinganishwa na wa nchi za Ulaya na Marekani.
Utafiti kuhusu Afrika nchini China ulianzia miaka ya 1950, yaani baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.
Ilipofika miaka ya 1960, nchi nyingi za Afrika zilipata uhuru, hivyo utafiti unaohusu Afrika nchini China ulianza kupamba moto.
Ilipofika mwaka 2000 FOCAC iliasisiwa hivyo ikaonekana kwamba utafiti unaohusu Afrika nchini China ulifungua ukurasa mpya na kuchangia maendeleo.
“Taasisi mpya zilijengwa na weledi wengi wapya walianza kuchangia utafiti kuhusu Afrika. Wachina walianza kufanya utafiti juu ya fani mbalimbali zinazohusu Afrika, zikiwemo historia, uchumi, siasa, anthropolojia, isimu, fasihi na nyinginezo.
Vilevile Barani Afrika, wanachuoni wengi zaidi walianza kutafiti mambo ya Kichina ili kuwajulisha Waafrika habari za China.
Wanazuoni wanabeba jukumu la kuchunguza na kufafanua undani wa utamaduni. Hivyo katika miaka ya hivi karibuni, wanazuoni wa China wameitilia maanani utafiti wa historia ya Afrika.
Hivyo mwaka 2021, Profesa Li Anshan alichapisha kitabu kipya kiitwacho Historia ya Kisasa ya Afrika, ambacho kilieleza jinsi Afrika ilivyojitahidi kutimiza maendeleo ya kisasa.
“Pia wasomi wa China wanajaribu kulinganisha utamaduni wa China na wa Afrika, kama vile dhana ya Confucianism ya China na dhana ya Ubantu ya Afrika,”.
Zaidi ya hayo, nchini China, wasomi wametafsiri vitabu vingi vya wanahistoria, wanafalsafa na wanasosholojia wa Afrika ili kuwajulisha Wachina fikra za watu wa Afrika, vilevile hali ya sasa na maendeleo ya Afrika.Wanachuoni wanabeba jukumu la kuhimiza mawasiliano na mazungumzo.
Tangu kuasisiwa kwa FOCAC, wanazuoni wa China na Afrika wamekuwa wakijadiliana na kuwasiliana mara kwa mara.
Kwa mfano, tokea mwaka 2022 Mkutano wa Mazungumzo ya Ustaarabu kati ya China na Afrika umefanyika kwa miaka mitatu mfululizo, ambao umekuwa jukwaa muhimu la wanazuoni wa Afrika na China katika kujadiliana mada muhimu kama vile,
Mambo ya kisasa kwa njia ya Kichina, ushirikiano wenye ubora wa juu baina ya China na Afrika, na njia ya maendeleo ya bara la Afrika.
Kupitia njia hizo, watu wa China haswa vijana wanazidi kufahamu utamaduni wa Afrika. Wengine wanavutiwa kwenda Afrika kusafiri ili kujionea mandhari nzuri na mambo mbalimbali Barani Afrika.
Wanazuoni pia wanabeba jukumu la kuwatayarisha weledi watakaochangia ushirikiano baina ya Afrika na China.
Wanafundisha darasani, wanatoa mihadhara, wanawasimamia wanafunzi katika kufanya utafiti. Wamesaidia kuwatayarisha weledi wanaofahamu utamaduni wa China na Afrika.
Nchini China, vyuo vikuu saba vimeanzisha kozi za lugha za kienyeji za Afrika. Vinafundisha lugha, utamaduni na historia ya Afrika ili kusukuma mbele ushirikiano baina ya China na Afrika katika sekta za utamaduni, elimu, sayansi na nyinginezo.
Katika vyuo vikuu vya Afrika, idara za Kichina na taasisi za utafiti wa Kichina zimeanza kujengeka, hivyo Wasomi wa pande mbili wanawatayarisha “mabalozi” wapya watakaosukuma mbele ushirikiano na mawasiliano baina ya China na Afrika.
Tunaamini kwamba mustakabali wa mawasiliano ya utamaduni katika ya Afrika na China unajaa matumaini na fursa.
Wanazuoni wa pande mbili wanajaribu kutafuta njia mpya ya kuwasiliana, ili kuimarisha na kusukuma mbele uhusiano na ushirikiano kati ya China na Afrika.
Waandishi wa Makala hii ni Mkuu wa Kitivo cha Afrika, Li Hongfeng na Mwalimu wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing(BFSU), China Wei Yuanyuan,