MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TARI Kihinga Yainua Kilimo Cha Michikichi Kigoma
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TARI Kihinga Yainua Kilimo Cha Michikichi Kigoma
Habari

TARI Kihinga Yainua Kilimo Cha Michikichi Kigoma

Author
By Author
Share
4 Min Read

– Mbegu Milioni 18 Zazalishwa, Mafanikio Yavuma Kitaifa

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), imekuwa
mstari wa mbele katika kuzalisha mbegu bora za mchikichi aina ya Tenera, kutoa elimu ya kilimo bora kwa wakulima na maofisa ugani, na kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya michikichi.

Mkurugenzi wa Kituo Cha TARI kilichopo Kihinga mkoani Kigoma, Dkt. Filson Kagimbo amesema hayo katika banda la taasisi hiyo katika Maonesho ya 49 yanayoendelea Dar es Salaam.

Dkt. Kagimbo amesema TARI Kihinga kimezalisha mbegu bora zaidi ya milioni 18.5 tangu kuanzishwa kwake hadi kufikia Julai 2025.

“Tangu tulipoanza kazi ya uzalishaji Oktoba 2018 hadi sasa, tumezalisha mbegu 18,591,000 za michikichi bora aina ya Tenera, na kati ya hizo tumeotesha miche milioni 4.7, ambapo milioni 3.4 imekwishapandwa shambani,” amesema.

Amesema mafanikio hayo yamechangia kuongezeka kwa mashamba ya michikichi bora hadi kufikia jumla ya hekta 27,908 nchini kote.

“Hii ni hatua kubwa ya kimaendeleo ikilinganishwa na hali ya awali ambapo asilimia 90 ya miti ya michikichi nchini ilikuwa ni ya asili (aina ya Dura) isiyozalisha mafuta mengi kama Tenera, ambayo ilikuwa inapatikana kwa asilimia tisa tu,” amesema.

Mbali na uzalishaji wa mbegu, amesema TARI Kihinga pia imefanya kazi kubwa ya kutoa elimu ya kilimo bora kwa wadau mbalimbali.

Kwamba Kufikia Julai 2025, kituo hicho kimefanikiwa kuwafundisha wakulima 2,266 na maofisa ugani 276, lengo likiwa ni kuhakikisha elimu hiyo inasambazwa kwa wakulima wengi zaidi kupitia maofisa ugani waliopatiwa mafunzo hayo.

Kwa mujibu wa Dkt. Kagimbo, “Zao la michikichi halikuwahi kupewa kipaumbele kitaifa hadi mwaka 2018 lilipoorodheshwa rasmi na serikali kuwa moja ya mazao ya kimkakati. Hapo ndipo elimu ya zao hilo ilipoanza kufundishwa katika vyuo vya kilimo, jambo ambalo awali lilikuwa halipo kabisa.”

Amesema kituo hicho kimekuwa chachu ya uelewa kwa wanafunzi kutoka vyuo na shule mbalimbali.

Amesema tayari wanafunzi 96 kutoka vyuo vya kati na vyuo vikuu wamepatiwa mafunzo ya vitendo kuhusu kilimo cha michikichi, huku wanafunzi 214 wa sekondari nao wakinufaika na mafunzo hayo.

Kwa upande wa uhamasishaji, TARI Kihinga imetumia vyombo vya habari kwa nguvu. Mpaka sasa vipindi 88 vya televisheni na vipindi 60 vya redio vimerushwa hewani, sambamba na kuchapisha makala zaidi ya 180 kwenye magazeti na blog mbalimbali, vyote vikihamasisha uwekezaji katika kilimo na usindikaji wa zao la michikichi.

Amesema serikali nayo imeendelea kuunga mkono juhudi kwa kutoa ufadhili wa kifedha na sera. Kabla ya kuanzishwa kwa kituo hicho, mbegu bora zilikuwa zikiagizwa kutoka nje kwa gharama kubwa.

“Mche mmoja wa Tenera uliuzwa kati ya shilingi 6,000 hadi 15,000, kulingana na mteja. Sasa tunazalisha hapa nchini na kuwagawia wakulima bure, hatua ambayo imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 18.7,” amesema.

Kwa sasa, Tanzania inahitaji tani 650,000 za mafuta ya kula kwa mwaka. TARI inakadiria kuwa ili kufikia uzalishaji huo kupitia michikichi pekee, kuna haja ya kuwa na mashamba yasiyopungua hekta 162,500 Hadi sasa, hatua iliyofikiwa ya hekta 27,908 ni mwanzo mzuri kuelekea azma ya taifa ya kujitegemea kwa mafuta ya kula.

Kwa mafanikio haya, TARI Kihinga si tu kuwa chachu ya maendeleo ya kilimo cha michikichi nchini, bali pia ni kielelezo cha jinsi tafiti na sera madhubuti zinavyoweza kuleta tija ya kiuchumi na chakula kwa taifa.

Serikali, wakulima, wawekezaji na wadau wengine sasa wanahamasishwa kushirikiana zaidi kufanikisha lengo la taifa la uzalishaji wa mafuta ya kula unaojitegemea.

Katika kipindi cha miaka saba tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Kihinga kilichopo Kigoma, mapinduzi makubwa yameshuhudiwa katika uendelezaji wa zao la michikichi nchini Tanzania. Tangu Julai 2018,

You Might Also Like

Majaliwa: Anwani Za Makazi Kupunguza  Safari Kwa Viongozi

VETA Shinyanga Waja Na Mafunzo Ya Saluni, Mapambo, Urembo

Dkt. Adesina Wa AfD Avutiwa Na Mwenendo Uchumi Wa Tanzania

Wataalam wa “Visit Finland” Wabadilishana Uzoefu Kutangaza Utalii Duniani 

Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mchengerwa Apongeza Shule Ya Sekondari Kibaha Kwa Ufaulu Wa Hali Ya Juu
Next Article Vyombo vya Habari ni Kama Maji’ -Biteko 
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TSB Yasisitiza Umuhimu Kuwekeza Kwenye Uchakataji Wa Mkonge
Habari July 10, 2025
eGA Yatengeneza  Mifumo  Kurahisisha  Kazi
Habari July 10, 2025
July 10, 2025
Habari July 10, 2025
Wanafunzi, Watafiti, Wanataaluma Kujadili Dini, Utamaduni na Maisha ya Kisasa
Habari July 10, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?