Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: SERIKALI imetumia Sh. Bilioni 38.7 kwa ajili ya kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa ajili ya ununuzi, ugomboaji, utunzaji na usambazaji wa shehena za dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
Waziri wa Afya Jenista Mhagama amesema leo Januari 30, 2025 katika kuadhimisha Kilele cha Siku ya Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele duniani.
“Hapa nchini Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele inajihusisha zaidi na kudhibiti magonjwa matano ambayo ni matende na mabusha, trakoma, usubi, kichocho na minyoo.
“Kwa kuanzia Novemba hadi Disemba mwaka jana 2024. Halmashauri 130 zilifanya zoezi la kumezesha kingatiba za ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo,” amesema.
Amesema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele duniani yapo zaidi ya 21, ambayo husababishwa na vimelea mbalimbali ikiwa ni pamoja na minyoo, bacteria, virusi na fangasi.
Amesema udhibiti wa magonjwa hayo ni kwa kufanya kampeni za ugawaji kingatiba kwa walengwa kulingana na ugonjwa husika.
“Makundi ya walengwa hao ni pamoja na jamii nzima, watoto wenye umri wa kwenda shule kuanzia miaka mitano hadi 14 na makundi maalum yaliyo katika mazingira hatarishi dhidi ya magonjwa hayo,” amesema.
Amesema Serikali imewekeza kwenye magonjwa hayo kwa kushirikiana na wadau imeweza kupata fedha pamoja na dawa za kutibu na kukinga magonjwa hayo hapa nchini.
“Aidha, Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali kwa mwaka 2024 tumeweza kutoa dawa za kingatiba za kudhibiti na kutokomeza magonjwa hayo kama ifuatavyo.
“Watu 257,358 kati ya 265,217 walipatiwa kingatiba za kutokomeza ugonjwa wa matende na mabusha kutoka kwenye Halmashauri za Mtama na Mtwara
Mikindani sawa na asilimia 97,.
“Watu milioni 5,462,851 kati ya 6,447,157
kutoka katika halmashauri 24 walipatiwa kingatiba ya ugonjwa wa Usubi sawa na asilimia 85, watu milioni 1,603,425 kati ya 1,967,143 kutoka Halmashauri saba za Ngorongoro DC, Monduli DC, Longido DC, Kiteto
DC, Simanjiro DC, Mpwapwa DC na Kalambo DC, walipatiwa kingatiba za ugonjwa wa trakoma,” amesema.

Amesema watoto wenye umri wa kwenda
shule yaani umri wa miaka 5 hadi 14 , 9,896,694 walilengwa kupatiwa huduma ya
kingatiba kwa ugonjwa wa minyoo ya tumbo ambapo hadi kufikia Disemba 2024 Watoto 8,676,234 sawa na asilimia 88 walimeza kingatiba.

Aidha, kwa ugonjwa wa kichocho walengwa wa kumeza kingatiba walikuwa 8,145,947 kati ya hao watoto 6,289,884 sawa na asilimia 77 walimeza
Kingatiba tajwa.
Kingatiba tajwa.
Walengwa hawa walifikiwa katika Halmashauri 171 sawa na asilimia 93 ya Halmashauri zote.
“Serikali kwa kushirikiana na wadau hutoa huduma kwa wananchi ambao tayari wamepata athari za magonjwa hayo ikiwemo upasuaji kwa watu wenye
tatizo la ugonjwa wa mabusha ambapo kwa mwaka 2024 watu wapatao 1,084 wamepatiwa huduma ya upasuaji,
tatizo la ugonjwa wa mabusha ambapo kwa mwaka 2024 watu wapatao 1,084 wamepatiwa huduma ya upasuaji,
“Na takriban wagonjwa 2,412 sawa na
asilimia 67 ya matarajio wenye tatizo la Vikope wamerekebishwa kope bila
malipo.,” amesema.
asilimia 67 ya matarajio wenye tatizo la Vikope wamerekebishwa kope bila
malipo.,” amesema.
Amesema Miongoni mwa malengo ya Serikali ni kuendelea kutumia rasilimali chache zilizopo katika kudhibiti magonjwa yanayowasumbua wananchi wake.