- Ni Katika Maonesho Ya Nchi Za Kimataifa Ya Biashara China
Na Waandishi Wetu
MAONESHO ya Saba ya Uingizaji ya Kimataifa ya China yalifunguliwa rasmi Novemba tano, 2024 – Shanghai China.
Katika maonesho hayo China ikiwa mwenyeji, Nchi ya Tanzania iliweza kujizolea umaarufu mkubwa.
Mwalimu wa Lugha ya Kiswahil kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU) Ning Yi, katika makala haya anasema kwamba, umaarufu huo wa Tanzania umetokana na faida yake kijiografia na uwepo wa rasilimali nyingi za asili ulichochea umaarufu katika maonesho hayo.
Hivyo ikaimarisha na kuleta nguvu mpya katika ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Tanzania.
Mojawapo ya kivutio ni“Dhahabu Nyeusi” ya Tanzania—Harufu ya Kahawa Yafika Shanghai.
Mwandishi wa makala haya, anasema kahawa ya Tanzania inajulikana duniani kwa ladha yake ya kipekee na utamu wake wa ajabu na inajivunia sifa moja ijulikanayo kama “Dhahabu Nyeusi”.
Kwamba mashamba yaliyopo maeneo ulipo Mlima Kilimanjaro yaliyojaa ardhi ya volkano yenye rutuba hutoa punje bora ya kahawa ambayo yameipa kahawa ya Tanzania sifa ya “Mfalme wa Kahawa ya Afrika”.
Ning anasema katika Maonyesho ya Sita ya Uingizaji ya Kimataifa ya China, kampuni moja ya utengenezaji wa kahawa kutoka Tanzania ilifanikiwa kupata wasambazaji wa kahawa nchini China, na kufungua soko kubwa la China kwa bidhaa zake.
Anasema Mwaka wa 2024, kampuni hiyo imejitokeza tena katika maonyesho na kupeleka bidhaa mpya zaidi.
Kadri soko la kahawa linavyoendelea kupanuka nchini China, mauzo ya kahawa ya Tanzania yanatarajiwa kuongezeka.
Pia Tanzania haikuishia kwenye kahawa pekee, pia kwenye Mwani uliopewa jina la “Dhahabu ya Kijani” Kutoka Zanzibar—Mwani Wakuza Ajira kwa Wanawake wa Zanzibar.
Mwani ni bidhaa maalum inayozalishwa kwa wingi kisiwani Zanzibar, ambayo inaweza kutumika moja kwa moja kama saladi au kama malighafi ya viwanda.
Kufikia mwishoni mwa mwaka 2022, uzalishaji wa zao la mwani ulikuwa umezidi tani 12,000 kwa mwaka huko Zanzibar.
Ning anasema kwa sababu ya thamani yake ya kipekee ya virutubisho na faida za kimatibabu, mwani unaitwa “Dhahabu ya Kijani” na wakazi wa Zanzibar.
Mwani hautumiki kwenye chakula pekee bali hutumika pia kwenye vipodozi, dawa na vitu vinginevyo.
Katika Maonesho hayo makubwa, bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na mwani zilikuwepo wakiwemo wafanyabishara wa Tanzania.
Bidhaa hizo zilivutia watu mbalimbali waliofika kwenye maonesho hayo.
Anasema bidhaa hizo hazionyeshi ustadi pekee wa ufundi wa jadi kutoka Zanzibar, lakini pia zilitengeneza fursa nyingi za ajira kwa wanawake wa Zanzibar.
Pia Mazao ya Korosho Yanavyoendelea kuongezwa thamani na kutoa bidhaa mbalimbali.
Nchi ya Tanzania ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa korosho duniani.
Katika miaka ya karibuni, korosho za Tanzania zimepata umaarufu mkubwa kwenye soko la China. Katika Maonyesho yaliyopita korosho za Tanzania zilikuwa moja ya bidhaa maarufu, na kuvutia wanunuzi wengi.
Mnamo mwaka 2021, kampuni moja ya biashara ya kimataifa kutoka Hunan, China, ilifanikiwa kupata uzabuni wa kuingiza korosho za Tanzania, na kuanzisha uhusiano mzuri wa biashara ya korosho kati ya China na Tanzania.
Maonyesho ya 2024 Yasaidia Kuinua Ushirikiano wa Biashara Kati ya China na Tanzania
Ning anasema mnamo mwaka 2023, biashara ya pande mbili kati ya China na Tanzania ilifikia Dola Bilioni 8.78, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.9 ikilinganishwa na mwaka 2022.
China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Tanzania kwa miaka minane mfululizo. Maonyesho ya Uingizaji ya Kimataifa ya China yamekuwa jukwaa bora kwa bidhaa za Tanzania kuingia kwenye soko la China, na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Vilevile anasema Tanzania na China zinafanya juhudi kubwa kupanua ushirikiano kati yao. Tanzania imepanua mauzo ya bidhaa za kilimo kwa China ili kuongeza pato la taifa.
Na kampuni za China zimefanikisha miradi ya reli, madaraja, bandari, mifumo ya huduma za maji na mingineyo nchini Tanzania, ikileta mabadiliko makubwa.
Bidhaa nyingi za kipekee za Tanzania ambazo awali hazikujulikana sana kwa walaji wa China sasa zimepata nafasi katika soko la China kupitia maonyesho ya kimataifa, na kuwa mfano hai wa ushirikiano wa kibiashara unaofaidisha pande zote mbili.
Mwandishi : Zhou Li, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Tianjin (TFSU)
Barua pepe: sylvanzhou@foxmail.com
Mwandishi 2: Ning Yi ni mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU)
Barua pepe:02706@shisu.edu.cn