- Na Waandishi Wetu
NOVEMBA mwaka jana 2024, mashindano ya kwanza ya Kimataifa ya Maandishi ya China na Afrika, yaliyoandaliwa na Mtandao wa Utafiti wa China-Africa wa Shanghai (China-Africa Shanghai International Network – CASIN).
Mashindano ambayo yalifanyika kwa mafanikio, yakiwa na lengo la kutoa uelewano mpya wa kifasihi kwa maingiliano na urafiki kati ya watu wa China na Afrika.
Kuonyesha umuhimu wake walihimizwa watu wengi kushiriki katika mijadala kuhusu uhusiano wa China na Afrika.
CASIN ni tawi la kienyeji la mtandao wa utafiti wa wachina barani Afrika nchini China.
Hivyo kupitia mihadhara, mikutano ya pande mbalimbali na utafiti, CASIN inatoa nafasi za mawasiliano kwa wanafunzi na wataalamu wa Afrika, watafiti na wataalamu wa China wanaofanya kazi barani Afrika, na makundi mengine, ili kutoa maarifa ya moja kwa moja katika kuelewa uhusiano wa China na Afrika na kukuza mazungumzo ya kimataifa baina ya pande hizo.
Tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mwaka 2000, mijadala kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika inahusiana na mada kuu mbili za siasa na uchumi, haswa katika vyombo vya habari na uwanja wa kitaaluma.
Ikilinganishwa na hali hii, mada ya kibinadamu katika mawasiliano ya China na Afrika haikutiwa maanani na mazungumzo makuu.
Katika muktadha huu, mashindano ya Kimataifa ya Maandishi ya China na Afrika yaliyoandaliwa na CASIN yalilenga kukuza uelewano wa uhusiano wa kijamii na mambo ya kihisia yenye utatanishi katika maingiliano kati ya watu wa China na Afrika.
Mashindano haya yalipokea mawasilisho 35 yaliyoandikwa kwa Kiingereza au Kichina, zikiwemo kazi 25 za kubuniwa na kazi 10 zisizo za kubuniwa.
Waandishi hao wanatoka nchi mbalimbali zikiwemo, China, Nigeria, Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Uganda, Botswana, Burundi, Madagascar na Mauritius.
Wengi wa waandishi hao ni vijana wa China wanaofanya kazi au waliowahi kufanya kazi barani Afrika, wanafunzi wa Kiafrika wanaosoma nchini China, na wanafunzi wanaotaka kufanya utafiti kuhusu uhusiano wa China na Afrika.
Hatimaye kazi tano za maandishi zilipata tuzo katika mashindano hayo, ikiwa ni pamoja na kazi zisizo za kubuniwa, na zile za kubuniwa.
Sasa kazi za Kiingereza na tafsiri za kazi za Kichina zimechapishwa kwenye tovuti ya ‘The Elephant’, mshirika wa Kiafrika wa mashindano hayo.
Mratibu wa mashindano na Profesa Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Jiaotong cha Shanghai, Shi Donglai (Flair), anasema,
“Tunatumai kuondoa ubaguzi na mipaka ya mawasiliano wa China na Afrika katika vyombo vya habari na umma kwa kupitia nguvu ya maandishi, bila kujali kuwa ubaguzi huo unatokana na mitazamo ya Ulaya au kutoka kwa maoni ya kitamaduni ya watu wa China na Afrika.”
Kwamba, Kazi za kifasihi zinaweza kuwasaidia wasomaji kuona uzima na utatanishi wa utu kwa kupitia kuonyesha ubaguzi na migogoro katika mawasiliano baina ya watu, ambao unavuka mipaka ya kitaifa.
Namna hiyo ya kuonyesha utu inajenga daraja la uelewano na mawasiliano kati ya watu kutoka tamaduni tofauti na kanda mbalimbali.
Katika zama za leo, utandawazi unaendelea kwa kina, uhusiano kati ya nchi duniani unazidi kuwa karibu, na kujenga Jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja ni mwelekeo usioepukika katika mchakato wa maendeleo ya China na Afrika.
Kwa kupitia kuonyesha maisha ya wachina barani Afrika au Waafrika nchini China kutokana na mitazamo tofauti, maandishi ya kifasihi yanaweza kushinda vikwazo vya kijiografia na kitamaduni, ili kuwezesha kuona watu wa China na Afrika wakitembea pamoja bila kujali umbali mrefu.
Hii inatoa uelewano mpya wa kibinadamu ili kuelewa ugomvi na urafiki kati ya China na Afrika, na pia inaongeza nguvu zaidi katika kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika na kukuza ujenzi wa Jumuiya ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja.
Mwandishi 1: Song Yiting, mwanafunzi wa shahada ya pili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).
Barua pepe:Yiting_Mo@126.com
Mwandishi 2: Ning Yi, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).
Barua pepe:02706@shisu.edu.cn