Na Waandishi Wetu
TEKNOLOJIA ya ubunifu kutoka nchini China imewezesha ufanikishaji wa upasuaji wa kisasa usiohitaji kufungua kifua kwa watoto waliokuwa na matatizo ya moyo tangia walipozaliwa.
Ubunifu huo uliripotiwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam iliyopo nchini Tanzania katika siku za karibuni baada ya watoto watano kufanyiwa upasuaji huo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyom upasuaji huo ulifanywa na timu ya pamoja ya madaktari wa China na Tanzania kwa kutumia teknolojia ya ubunifu kutoka China.
Kwamba, Mbinu hiyo ya upasuaji wa ndani kwa kutumia mwongozo wa mawimbi ya sauti, ilibuniwa na Profesa Pan Xiangbin na timu yake kutoka Hospitali ya Fu Wai,
Teknolojia hiyo, huondoa hitaji la kufungua kifua, huepusha madhara ya mionzi, hupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za matibabu, na inaweza kufanyika hata katika maeneo ya mbali kwa kutumia magari maalum ya huduma ya matibabu inayotembea.
Kwa kutumia teknolojia hiyo inatoa matumaini ya maisha yenye afya bora kwa watoto wenye umri kati ya miaka mitatu hadi saba.
Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge ameeleza ikiwa teknolojia hiyo itasambazwa kwa kiwango kikubwa, idadi ya upasuaji kwa mwaka inaweza kuongezeka kutoka kwa wagonjwa 783 hadi zaidi ya 2,000.
Amesema teknolojia hiyo itakuwa hatua muhimu katika kuinua ubora na kiwango cha ushirikiano wa kitabibu kati ya China na Tanzania.
Tangu miaka ya 1960 nchi ya China imekuwa ikitoa msaada wa kitabibu Barani Afrika na imeandika historia yenye mafanikio makubwa nchini Tanzania.
Jumla ya timu 27 za madaktari zimefika Tanzania Bara, na nyingine 33 visiwani Zanzibar, ambapo zimesaidia kutoa huduma kwa zaidi ya wagonjwa milioni 10. Zaidi ya mbinu 100 mpya za kitabibu ziliwasilishwa hadi Bara la Afrika.
Picha hii inaonyesha timu ya madaktari kutoka China ikifanya kliniki ya kuhamahama mnamo Aprili 2025 katika mkoa wa Arusha, Tanzania.
Kwa mujibu wa huduma zinazotolea na China nchini Tanzania, moja ya mafanikio ya kihistoria ni Mradi wa Kudhibiti na Kuzuia Ugonjwa wa Kichocho ulioanzishwa Zanzibar mwaka 2017.
Kwamba kupitia mradi huo timu ya wataalamu kutoka China ilisaidia kupunguza kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 8.92 hadi asilimia 0.64.
Kwa kutambua mchango huo wa kipekee, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, aliwatunukia wataalamu hao medali za heshima mnamo Agosti mwaka jana, 2024.
Timu ya madaktari kutoka China inaongozwa na falsafa ya ‘Afadhali kumfundisha mtu jinsi ya kuvua samaki kuliko kumpa samaki’ inasisitiza uendelevu wa huduma za afya kwa njia ya mafunzo kwa wataalamu wa ndani na uhamishaji wa teknolojia za kisasa.
Lengo kuu ni kusaidia Tanzania kuinua kiwango cha huduma zake za afya kwa msingi wa kujitegemea.
Hivyo Kwa zaidi ya miaka 60 msaada wa kitabibu wa China Barani Afrika umekuwa mfano bora wa ushirikiano wa afya kati ya pande hizo mbili.
Zaidi ya madaktari 25,000 wa China wametumwa katika nchi 48 za Afrika, wakichangia kikamilifu katika utekelezaji wa mpango wa ‘Njia ya Ushirikiano wa Kiafya’.
Chini ya mwongozo wa dhana ya kujenga kwa pamoja Jumuiya ya Afya ya Binadamu timu ya madaktari wa China itaendelea kushikilia moyo wa ‘kutojali hatari na kushikilia moyo wa kujitolea’, ikiendelea kushirikisha uzoefu wao wa kuzuia na kudhibiti magonjwa, kubuni mbinu mpya za ushirikiano wa kitabibu, na kutoa msukumo wa kudumu wa kuimarisha uimara wa mifumo ya afya ya umma barani Afrika,
Pia kuinua afya na ustawi wa watu wake, na kuendelea kuandika sura mpya ya ushirikiano wa kujenga kwa pamoja Jumuiya ya China – Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja.
Chini ya mwongozo wa dhana ya kujenga kwa pamoja Jumuiya ya Afya ya Binadamu, timu ya madaktari wa China itaendelea kuonyesha moyo wa dhati, kujitolea, na mshikamano.
Kwa kushirikiana uzoefu katika kuzuia na kudhibiti magonjwa, na kubuni mbinu bunifu za ushirikiano wa afya, wataendelea kuchangia katika kuimarisha ujenzi wa mfumo wa afya ya umma barani Afrika, kuinua viwango vya huduma za afya katika nchi za Afrika, na kufungua sura mpya ya Jumuiya ya China – Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja.

Barua pepe:Yiting_Mo@126.com
Mwandishi Ning Yi, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).
Barua pepe:02706@shisu.edu.cn