Na Waandishi Wetu
SOYA ni jamii ya kunde ni zao lenye mafuta na sifa yake pekee ni kuwa na kiasi kikubwa cha protini.
Maziwa yatokanayo na soya yana asili yake nchini China ambapo zao hilo limetokea, baadaye zao hilo na vyakula vyake vilikwenda Japani, kisha kusambaa ulimwenguni kote.
Maziwa ya soya ni kinywaji cha kiasili cha Kichina chenye ladha ya kipekee na kiasi kikubwa cha lishe, wengine wanaipendelea kwa sababu za kiafya.
Mradi wa kukuza maziwa ya soya nchini Tanzania unaitwa “Soya Ndogo, Lishe Bora”. Kwa kufuata utekelezaji wa mradi huo, kinywaji hicho cha “Kichina” kimevuka milima na mito na kufika kwenye Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania, kikiwa kinywaji kipya kinachosaidia kujenga afya.
Hivyo kimechangia kukuza maendeleo na mambo ya kisasa katika kujenga Jumuiya ya China – Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja.
Katika kudhihirisha kuwa kinywaji hicho kimechangia maendeleo miongoni mwa China na Afrika, tokea mwaka 2011 Chuo Kikuu cha Kilimo cha China (CAU) kimekuwa kikishirikiana na Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania kutekeleza mradi wa ‘Teknolojia Ndogo, Mavuno Makubwa’.
Mradi huo unalenga kuongeza uzalishaji wa mahindi na mapato ya wakulima, na kuhamasisha “uzoefu wa China” wa kuongeza uzalishaji wa mahindi kwa upandaji wa karibu.
Mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa, na mapato ya wakulima yameongezeka kwa kiasi kikubwa.
Kwamba Mradi huo umepewa tuzo ya ‘Mfano Bora wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini’ na Umoja wa Mataifa, na umejumuishwa katika Mradi wa Kupunguza Umaskini na Kuleta Faida za Kilimo kati ya Miradi Tisa ya Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) mwaka 2021.
Mnamo mwaka 2021, Chuo Kikuu cha Kilimo cha China kiliboresha mradi wa ‘Teknolojia Ndogo, Mavuno Makubwa’ kuwa mradi wa pamoja wa ‘Soya Ndogo, Lishe Bora’, na kuchagua vijiji vinne kuanzisha mradi huo kama vijiji vya mfano.
Kupitia kilimo cha mazao mchanganyiko ya mahindi na soya, mradi huo umeifanya ardhi kuwa na rutuba zaidi na kuboresha ufanisi wa matumizi ya ardhi kwa jumla.
Kama matokeo ya mradi huo, mavuno ya soya yaliongezeka kutoka takriban kilo 100 kwa ekari hadi kilo 533 kwa ekari.
Pia mradi huo unawafundisha wakulima wa Afrika utengenezaji wa maziwa ya soya, usindikaji wa mazao ya soya na teknolojia nyingine nyingi, ambazo sio tu zinaboresha lishe na afya za watu, lakini pia zinachochea uundaji na maendeleo ya michakato kamili ya biashara kutoka upandaji hadi uzalishaji, usindikaji na uuzaji.
Kwamba Mradi huo unaelezea kwa ufanisi maana kubwa ya kupunguza umaskini na kuleta faida za kilimo, ni mfano mwingine wa maendeleo na ushirikiano wa kilimo kati ya China na Afrika.
Agosti mwaka jana 2024, mradi wa Teknolojia Ndogo, Mavuno Makubwa: Soya Ndogo, Lishe Bora wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China ulionyeshwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Tanzania.
Katika maonyesho hayo, wakazi na maofisa kutoka vijiji vinavyoshiriki mradi huo walionesha namna ya kupukuchua mahindi kwa mikono na kutengeneza maziwa ya soya kwa kutumia kinu, mbinu ambazo walijifunza kutoka kwa timu ya Wachina.
Jambo hilo liliwavutia watazamaji wengi, wakiwemo maofisa wa kilimo, wahadhiri wa teknolojia za kilimo na wakulima wawakilishi kutoka nchini Tanzania.
Pia Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania,Mizengo Pinda, alivutiwa na kutazama kwa makini mchakato wa kutengeneza maziwa ya soya.
Utekelezaji wa mafanikio wa mradi wa Soya Ndogo, Lishe Bora” ni mfano mzuri wa kushirikisha uzoefu wa China katika maendeleo ya kilimo na kupunguza umaskini nchini Tanzania.
Huu sio tu unatatua tatizo la upungufu wa ulaji wa protini, bali pia unaleta fursa mpya kwa wakulima kuongeza mapato yao, na kufurahisha upatikanaji wa lishe bora kwa waafrika.
Katika siku zijazo, miradi mingi zaidi ya ushirikiano wa Kusini-Kusini ukiweno wa Soya Ndogo, Lishe Bora utaendelea kuthibitisha urafiki wa China na Tanzania kwa vitendo halisi, kuimarisha dhamira ya pamoja ya China na Afrika kushirikiana kuendeleza mambo ya kisasa, na kuingiza nguvu mpya katika ujenzi wa Jumuiya ya China – Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja.
Mwandishi : Ning Yi, ni mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).
Barua pepe:02706@shisu.edu.cn
Mwandishi :Song Yiting, Mwanafunzi wa Shahada ya Pili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).
Barua pepe:Yiting_Mo@126.com