Na Lucy Lyatuu
WAKALA wa Usajili wa Biashara na leseni (BRELA) wameibuka washindi wa kwanza wa jumla na kupewa tuzo katika kundi la Uwezeshaji wa Biashara na Uwekezaji katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Dar es salaam.
Brela iliibuka mshindi wa kwanza Julai 7,2025 katika ufunguzi wa maonesho hayo yaliyofunguliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi.
Seka Kasera Meneja wa alama za Biashara ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela amewashukuru watumishi wenzake wa berla kwa ushirikiano waliouonesha katika maonesho hayo hadi kuibuka washindi na kupata tuzo hiyo.
”Tunawahakikishia wateja wetu tutaendelea kuwahudumia Wananchi hata nje ya sabasaba hivyo wateja wetu wasiwe na wasiwasi” amesema Kasera.
Amewataka wananchi waendelee kuja katika maonesho ya sabasaba kwani usajili unafanyika wa papo kwa hapo na wateja wote watahudumiwa kwa kadiri itakavyotakiwa.
”tuzo hii hatukupata kwa bahati mbaya, tulistahili kwani watumishi wenzangu wa Brela walianza kuwahudumia wateja tangu siku ya kwanza katikla maonesho hayo mpaka leo wateja walikuwa wakimiminika kupatiwa huduma”, amesema Kasera”