Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: WIZARA ya Katiba na Sheria inapokea malalamiko ya mwananchi ambaye hajatendewa haki mahakamani au kwenye eneo lolote linalohusiana na haki.
Wakili wa Serikali kutoka Kitengo cha Katiba na Ufuatiliaji Haki wizarani hapo, Doris Dario amesema hayo kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam.
Amesema, ” Tunapokea malalamiko yale, tunayafanyia kazi, tunawasiliana na taasisi husika au wizara husika, suala hilo linapatiwa ufumbuzi.
“Na kuna masuala mengine tunayapokea yanakuwa na udharura, labda mwananchi anaona lkama hajatendewa haki kwa hiyo tunawasiliana na eneo husika kutaka kujua, suala linafanyiwa kazi na kutoa mrejesho, kisha tunawasiliana na mwananchi,” amesema.
Kwa upande mwingine amesema jatika maonesho hayo wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi ili wajue mifumo ya utoaji haki, lakini wajue wajibu na haki yao, kwa mujibu wa katiba.
“Inapotokea mtu ametendewa sintofafamu basi ajue wapi pa kupeleka changamoto yake. Katika ngazi zile za kimahakama au katika vyombo vingine ambavyo vinapokea malalamiko ya wananch,” amesema.