Na Waandishi Wetu
UTOZAJI kodi ya juu umechochea migogoro ya kibiashara duniani, jambo hilo limejitokeza katika kipindi cha muhula wa pili kwa Rais wa Marekani Donald Trump.
Jambo hilo limechangia kuonekana kwa athari kwenye maeneo mbalimbali nchini Marekani.
Kwa kuwa thamani za hisa katika masoko ya fedha ya Marekani zilishuka, na sarafu ya dola na dhamana za serikali ya Marekani ziliuzwa kwa kiasi kikubwa kipindi fulani.
Kutokana na hali hiyo, Jumuiya ya wafanyabiashara ya Marekani inalalamika, upinzani wa kisiasa unaendelea, huku mbinu za serikali ya Marekani kushinikiza nchi nyingine zikikumbana na vikwazo.
Afrika ni miongoni mwa eneo lililoathirika kutokana na mvutano huo wa ushuru wa forodha.
Marekani imeweka ushuru wa zaidi ya asilimia 10 kwa uchumi mdogo na nchi maskini zaidi.
Lesotho imelazimishwa kutozwa ushuru wa kiwango cha juu cha asilimia 50.
Kama moja ya nchi maskini zaidi, Lesotho zinauza zaidi ya nusu ya mavazi yake kwa Marekani.
Hivyo sera mpya za ushuru wa forodha za Marekani zitasababisha kuanguka kwa sekta yake ya usindikaji wa mavazi na idadi kubwa ya wafanyakazi kupoteza kazi.
Uchumi wa nchi za Afrika ni mdogo na una muundo wa kipekee, na uwezo wao wa kukabiliana na hatari ni dhaifu.
Ushuru mkubwa umezidi kiwango ambacho nchi za Afrika zinaweza kuvumilia.

Msomi kutoka nchini Tanzania,
Benedict Huruma Mwakabungu, anasema sera mpya za ushuru za Marekani sio tu zimekiuka kanuni husika za Shirika la Biashara Duniani(WTO), bali pia zimepuuza sheria za kimsingi za uchumi.
Pia kuzifanya gharama za kufanya biashara kati ya nchi za Afrika na Marekani zipande kwa kasi.
Ili kutatua changamoto hizi, anapendekeza makampuni ya Afrika kurekebisha mikakati yao kwa njia ya kuangalia masoko ya nchi nyingine kama China, na kutafuta fursa mpya za ushirikiano kwa kupanua masoko ya nje.
Mbali na kuongeza ushuru wa forodha, utawala wa Rais Trump umekatisha msaada wa mabilioni ya dola za kimarekani kwa Afrika, kwa kufunga Shirika la ‘Misaada la ‘Millenium Challenge Corporation’
na kusababisha miradi ya miundombinu nchini Niger, Msumbiji kusitishwa.
Vilevile, ulitishia kutosaini tena Mpango wa Ukuaji na Fursa wa Afrika ( AGOA) na kudhoofisha zaidi biashara ya nje ya Afrika.
Hivyo Nchi za Afrika zinapaswa kutegemea kikamilifu kazi za eneo la Biashara Huria Afrika, kuharakisha ushirikiano wa biashara ndani ya eneo hilo na kufungua masoko mapya, ili kujiondoa katika tatizo hilo.
Wachambuzi wa kisiasa wa Afrika Kusini wanaamini kuwa, kuimarika kwa uhusiano wa kiuchumi wa Afrika na mataifa mengine kutaifanya Marekani kuwa mbali zaidi na jamii ya kimataifa.
Wakati China inapozidisha ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na kufanya kazi na mataifa mengine kuendeleza mambo ya kisasa, Marekani inaanzisha vita vya ushuru na kusukuma nchi nyingi kuelekea upande mwingine.
Vitendo hivyo vya Marekani sio tu vinadhuru maslahi ya nchi nyingine, lakini pia vinaweza kuleta madhara kwa nchi hiyo.
Wakati huo huo, juhudi za nchi za Afrika za kuchunguza njia mpya za maendeleo zimebainisha kuwa ushirikiano wa kimataifa na faida ya pande zote ndio mwelekeo halisi wa maendeleo ya dunia.

Ning Yi, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).
Barua pepe:02706@shisu.edu.cn
Ye Tianfa, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Tianjin (TFSU)
Barua pepe: tianfa202123@163.com