MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kamati Ya Uongozi Wa Miradi Wa JNHPP Yakagua Maendeleo Ya Bwawa La Julius Nyerere
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kamati Ya Uongozi Wa Miradi Wa JNHPP Yakagua Maendeleo Ya Bwawa La Julius Nyerere
Habari

Kamati Ya Uongozi Wa Miradi Wa JNHPP Yakagua Maendeleo Ya Bwawa La Julius Nyerere

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Uongozi wa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), imekagua maendeleo ya uzalishaji wa umeme katika bwawa la Julius Nyerere na kueleza kuridhishwa na usimamizi pamoja na utekelezaji wake, uliokidhi viwango vya ubora vinavyoendana na thamani ya fedha iliyowekezwa na Serikali.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi , amesema kamati imefurahishwa na namna bwawa hilo linavyochochea ukuaji wa uchumi kwa kuongeza uzalishaji wa umeme unaosambazwa katika maeneo mbalimbali nchini, hatua inayochangia kuimarika kwa upatikanaji wa nishati ya umeme.

“Tumeridhishwa na jinsi mradi huu ulivyosimamiwa na kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa. Ukilinganisha na miradi mingine barani Afrika, mradi huu umejengwa kwa ubora wa hali ya juu na umeleta unafuu katika huduma ya umeme nchini. Haya ni mafanikio makubwa kwa Taifa,” ameeeleza Dkt. Yonazi.

Habari Picha 11317

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Petro Lyatuu, amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 na mchango wake tayari umeanza kuonekana.

Amefafanua kuwa mwaka 2021, gridi ya taifa ilikuwa na jumla ya megawati 1,600, lakini kwa sasa uwezo wa uzalishaji umefikia zaidi ya megawati 4,000, zaidi ya mara mbili ya kiwango cha awali.

Habari Picha 11318

“Kwa sasa bwawa linazalisha umeme na tija yake imeonekana wazi. Kuongezeka kwa uzalishaji kumeimarisha gridi ya taifa na tunaendelea kuongeza nguvu katika sekta ya nishati kwa ajili ya maendeleo ya nchi na ustawi wa wananchi,” amesisitiza Lyatuu.

Aidha, awali, Kamati hiyo ilitembelea kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Chalinze, kinachopokea umeme kutoka Bwawa la Julius Nyerere na kusambaza katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji, Antony Mbushi, amesema kituo hicho kimekamilika na tayari kinafanya kazi.

Ameongeza kuwa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma umefikia asilimia 71.58, huku mradi wa kusafirisha umeme kutoka Chalinze kupitia Kinyerezi hadi Mkuranga umefikia asilimia 59.76.

‘’Kamati imeridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo na kusisitiza kuwa mpango uliopo ni kuendelea kuongeza uzalishaji ili kuhakikisha nishati ya umeme inakuwa ya uhakika na endelevu’,’ Ameongeza Mbushi.

Katika hitimisho la ziara hiyo, Kamati imeeleza kuwa utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya umeme unaifanya Tanzania kuwa kivutio cha uwekezaji na kitovu cha usambazaji wa umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini.

You Might Also Like

Ujenzi Miundombinu ya Kuongeza Udahili kipaumbele Cha Serikali
Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Waandishi Watakiwa Kuandika Kwa Usahihi
Kutofuata sheria chanzo kikuu cha migogoro ya kazi – CMA
Serikali Yaweka Utaratibu Biashara Pembezoni mwa Barabara
Tanzania, Japan Kushirikiana Ukuzaji Ujuzi Kwa Vijana
Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article PPAA Yazuia Utoaji Wa Tuzo Za Zabuni 43
Leave a Comment Leave a Comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Advertise

  • Advertise with us
  • Newsletters
  • Deal
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account