MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TFS Yang’ara Kitaifa Yashinda Tuzo ya Umahiri Uhifadhi Misitu Na Bayoanuai
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TFS Yang’ara Kitaifa Yashinda Tuzo ya Umahiri Uhifadhi Misitu Na Bayoanuai
Habari

TFS Yang’ara Kitaifa Yashinda Tuzo ya Umahiri Uhifadhi Misitu Na Bayoanuai

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeandika historia mpya katika sekta ya maliasili baada ya kushinda Tuzo ya Umahiri katika Uhifadhi wa Misitu na Ulinzi wa Bioanwai kwa mwaka 2025, tuzo inayotambua taasisi zilizoonesha matokeo chanya na endelevu katika kulinda rasilimali za asili.

Tuzo hiyo, inayojulikana kama Best Forest Conservation and Biodiversity Protection Award (TPSIA) 2025, imetolewa jana, Desemba 16, 2025, jijini Dar es Salaam katika hafla maalumu iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City.

Hafla hiyo iliandaliwa na Tanzania Professional Skills and Innovation Awards (TPSIA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo na sekta binafsi, kwa lengo la kutambua na kuthamini mchango na jitihada za taasisi za umma katika maendeleo ya taifa.

Katika hafla hiyo, tuzo ilikabidhiwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Uwekezaji ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Sharif A. Sharif.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi, Emmanuel Wilfred, alisema ushindi huo ni uthibitisho wa juhudi kubwa zinazofanywa na wakala huo katika kusimamia misitu na kulinda bioanwai kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo.

Habari Picha 10563

“Tunawashukuru waandaaji wa tuzo hizi kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na TFS katika uhifadhi wa misitu, ulinzi wa bioanwai na usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu. Ushindi huu ni ishara kuwa jitihada zetu zinaonekana na kuthaminiwa,” alisema Wilfred.

Aliongeza kuwa tuzo hiyo ni chachu ya kuongeza kasi ya utendaji, ikiwamo kuimarisha mapambano dhidi ya uharibifu wa misitu, uvunaji haramu, pamoja na kuendeleza ushirikishwaji wa jamii katika uhifadhi.

“Tuzo hii inatupa motisha ya kufanya kazi kwa bidii zaidi, kwa weledi na kwa uwajibikaji mkubwa ili kuhakikisha misitu ya Tanzania inalindwa na kuendelea kuwa nguzo ya uchumi, mazingira na ustawi wa wananchi,” aliongeza.

Kwa mujibu wa waandaaji wa TPSIA, TFS imechaguliwa kutokana na matokeo halisi ya utekelezaji wa sera na mikakati ya uhifadhi, ikiwamo kuimarika kwa ulinzi wa hifadhi za misitu, ongezeko la mapato yatokanayo na misitu, na mchango wake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

 

You Might Also Like

Hivi Ndivyo Vipaumbele Vya Maliasili

BOT Yatoa Elimu ya Uwekezaji, Fedha Kwa Wananchi Maonyesho ya Madini Geita

Zungu Achaguliwa Kuwa Spika Mpya Wa Bunge La 13

Mgombea NCCR-Mageuzi Awaasa Watanzania Wasikubali Propaganda

Bodi Ya  Bima Ya Amana Yapata Mkurugenzi  Mkuu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Spika Zungu Atangaza Kifo Cha Mbunge Wa Peramiho, Jenista Mhagama
Next Article Maofisa Habari Wa Serikali Jipangeni  Kiteknolojia- Katibu Mkuu Kiongozi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CAG Aipongeza TARURA Kwa Ujenzi Wa Miundombinu
Habari January 9, 2026
Tuna Deni La Kusimamia Miradi Na Kusikiliza Kero za wananchi Ili Kuleta Maendeleo Ya Kweli-Salome
Habari January 9, 2026
Rais Dkt Samia Azindua Majengo Ya Kisasa
Habari January 8, 2026
TEA, UNICEF Watekeleza Miradi ya Elimu Visawani Zanzibar
Habari January 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?