Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF Tanzania) imezindua rasmi utekelezaji wa miradi ya elimu visiwani Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA), ikiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya shule.
Kupitia ushirikiano huu, TEA na UNICEF wametenga jumla ya Sh. Bilioni 2.5 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa, maabara za sayansi, pamoja na matundu ya vyoo katika shule 20.
Shule 11 zipo kisiwani Unguja na shule 9 kisiwani Pemba.
Akizungumza kwenye kikao kazi cha mradi, Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha, alisema utekelezaji unatarajiwa kuanza mwishoni mwa Januari na kukamilika kabla ya mwezi wa sita mwaka huu, 2026.
Alibainisha kuwa lengo ni kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora, salama, na rafiki kwa afya zao.
Dkt. Kipesha pia alisisitiza kuwa TEA, kama taasisi ya Muungano, ina wajibu wa kutekeleza miradi ya elimu Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khamis Said akifafanua jambo katika kikao kazi maalum cha kujadili utekelezaji wa miradi ya elimu kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Mkuu wa WEMA, Khamis Said, aliishukuru TEA kwa mchango wake na kueleza kuwa miradi hiyo imechochea wadau wengine kuchangia maendeleo ya elimu.
Aliongeza kuwa ujenzi na ukarabati umefika wakati muafaka,

